Ni bilionea ambaye anajishughulisha na vitu mbalimbali, Bw. Elon Musk na sasa ameamua kuishangaza duniani kwa kuamua kujenga betri kubwa kuliko zote duniani ambalo litatumika kuzalisha umeme na wananchi hawatalipia hata shilingi kupata huduma hiyo 🙄 🙄 .
Kwa miaka kadhaa sasa Bw. Elon Musk ameamua kujikita zaidi katika utengenezaji wa vitu mbalimbali ambavyo vitaweza kusaidia watu wa hali ya chini. Na sasa yupo katika mpango wa kukamilisha kutengeneza betri kubwa kuliko yote kwa kushirikiana na Neoen (muundaji wa nishati inayoweza kutumika tena na tena wa Ufaransa) pamoja na serikali ya Australia.
Ushirikiano wa Musk na Neoen katika ujenzi wa betri kubwa zaidi duniani.
Katika makubaliano ya Bw. Musk na Neoen ni kwamba Tesla itajenga betri hiyo (mpaka sasa limeshakamilika kwa 50%) na kwa upande wa Neoen, mitambo yake inayotumia nishati ya upepo itatumia betri hiyo kuzalisha umeme. Betri hilo la aina ya Lithium-ion lina nguvu kiasi cha megawatt 100.
Katika mpango huo pia utahusisha uwekejaji wa jenereta za dharura ambazo zitatumika kuongeza ufanisi wa vyanzo vingine vya umeme kama vile kinu cha kuzalisha umeme kinachotumia nishati ya umeme wa Jua, umeme wa gesi.
Betri hilo likikamilika litakuwa limewasaidia wananchi kutolipa kiasi cha jumla ya $50 milioni kwa mwaka kuhakikisha wanapata nishati ya umeme kutokana na kwamba huduma hiyo itakuwa ikipatikana bure huko Kusini mwa Australia.
Vyanzo: The news in color, mitandao mbalimbali
2 Comments
Comments are closed.