Jinsi ya Kulazimisha Simu Ikae Kwenye 2G, 3G, au 4G tuu #Maujanja

1
Sambaza

Leo nitakufundisha jinsi gani ya kulazimisha moja kwa moja simu yako kupokea signo za mfumo wa aina flani tuu, – yaani 2G (GSM), 3G (WCDMA), 4G au vyovyote vile utakavyopendelea.

2G-3G-4G-TANZANIAKwa siku kadhaa nimekuwa nikitumia mtandao wa Smart ambao tumefanikiwa kuingia nao mkataba wa kutudhamini kwa huduma za intaneti na mawasiliano.

Changamoto ilikuja pale ambapo kwenye baadhi ya maeneo kutokana na sababu mbalimbali simu yangu inaondoa mfumo wa 4G na kwenda kwenye 3G bila ulazima. Inafanya hivyo kama signo za 4G zikiwa chini ingawa zikiwa zinatosha kabisa kwa kuendelea kunipa kiwango kizuri cha spidi ya kudownload ukilinganisha na mfumo wa 3G. Jambo ili likanifanya nichunguze kama kuna njia rahisi ya kulazimisha simu ipokee signo za 4G tuu.

SOMA PIA:  Jinsi gani unaweza kuigawanya diski uhifadhi #Maujanja

Kama nipo busy na kitu mfano kuangalia video za YouTube hili linakuwa tatizo, so nikaanza kuchambua kuhusu kulazimisha simu yangu ichukue signo za 4G tuu.

‘Simu kuhama hama signo za mtandao hutumia kiwango kikubwa cha chaji ya simu yako katika kuhama hama ukilinganisha na kama simu hiyo ikiwa inapokea signo ya aina moja tuu’

Kuna baadhi ya simu zinasehemu rahisi za kulazimisha hili katika eneo la settings (yaani mipangilio) lakini zingine zinakupa chaguo la kupendelea (prefer) 3G kama ipo na kama simu ikiona signo chache basi inakurudisha kwenye 2G. Leo nitakufundisha jinsi gani ya kulazimisha moja kwa moja simu yako kupokea signo za aina flani tuu, – yaani 2G (GSM), 3G (WCDMA), 4G au vyovyote vile utakavyopendelea.

SOMA PIA:  Ondoa tatizo la mafaili katika flashi kuonekana kama Shortcut

Hatua

> Kwenye sehemu ya kupiga simu (Dialer), andika na piga *#*#4636#*#* (hakikisha ni sahihi kama ilivyo), kisha piga.

> Itakuja chaguo – Ingia ‘Phone Information’,

Bofya 'Phone Information'

Bofya ‘Phone Information’

> Kisha ingia ‘Preferred network type’

Muonekano katika mtandao wa Smart, kulingana na mtandao wako unaweza kuona orodha tofauti kidogo

Muonekano katika mtandao wa Smart, kulingana na mtandao wako unaweza kuona orodha tofauti kidogo

Kulingana na simu yako basi utaweza kuona machaguo mbalimbali.

Kwenye simu nyingi utaona GSM, WCDMA, na WCDMA preffered, kwa simu zenye uwezo wa LTE (4G) utaona pia LTE.

1. WCDMA prefferred – mpangilio huu utakuwa unapendelea signo za 3G ila kama hazipo basi simu itapokea signo za 2G

2. WCDMA only – mpangilio ni kulizamisha simu kupokea signo za 3G tuu na hivyo kama hazipo utakosa signo kabisa kwenye simu

SOMA PIA:  Hatua 5 za kubalisha akaunti ya Facebook kuwa ya kibiashara

3. GSM only – mpangilio huu utaweka simu kwenye mfumo wa 2G tuu. Mfumo huu ni mzuri kama hutumii huduma za intaneti sana/kabisa, kwani unatumia chaji ya simu kidogo sana

4. LTE/CDMA auto – mpangilio huu utafanya simu yako kuhama kati ya mfumo wa 3G na 4G kulingana na upatikanaji wa signo

> Chagua kulingana na upendavyo, mabadiliko yatatokea mara moja na kama hayajatokea basi zima na kuwasha simu na hilo litakuwa limefanyika.

Soma Pia – Fahamu Tofauti Kuu Kati ya Teknolojia za 2G, 3G, 4G n.k

Uwezo huu unapatikana zaidi kwenye simu nyingi za Android za kuanzia toleo la Android 4.4 na kuendelea. Ni simu chache tuu ndio watengenezaji wamezuia uwezo huo, jaribu na utuambie kama kwako umefanikiwa. Endelea kutembelea mtandao wa TeknoKona

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. ahamadi namenga on

    Simu yangu haiaccess whatsapp,, nikitumia Wi-Fi inakubali ila nikiweka mb za kawaida inakataa, inaniletea neno YOU MAY HAVE MESSAGES ON YOUR WHATSAPP.
    Nilijaribu ku-uninstall na kuinstall tena lakini haiwezekani.. Je nifanyeje ili ikubali. Tatizo lilianza baada ya kurestore simu. Natumia TECNO W3LTE

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com