AniMouse - Tumia Mouse Ya Laptop Bila Ya Kutumia Vidole - TeknoKona Teknolojia Tanzania

AniMouse – Tumia Mouse Ya Laptop Bila Ya Kutumia Vidole

0
Sambaza

Moja kati ya maendeleo yaliyofanyika katika kipindi cha miaka iliyopita ni jinsi ambavyo teknolojia inavyo weka urahisi wa watu kujichanganya na dunia nzima kwa ujumla.

buy clomid over the counter

 Kwa mfano kama mtu amezaliwa na ulemavu wa kusikia anaweza pata vifaa maalum vya kiteknolojia vitakavyoweza kumuwezesha kusikia bila shida yeyote.

Kama mtu hawezi tembea pia kuna vifaa maalumu vya kumuwezesha kutembea (exoskeletons). Kuna mambo mengi sana yaliyorahishishwa kwa kutumia teknolojia. Hata kama una wakati mgumu katika kuhamisha mouse ya komyuta yako, kuna njia ya kukuwezesha kutumia mouse (kwa kutumia Animouse) hiyo bila shida yoyote.

Njia hii itafanya kazi kwa wale wanaopata wakati mgumu katika kutumia mouse za kompyuta zao (laptop sana sana) na hii ikijumuisha hata wale ambao mouse zao za laptop zimekufa

Programu moja ya bure na rahisi kutumia inayoitwa Animouse itakuwezesha kufanya hivyo. Programu hii imeanzishwa na mvulana mdogo tuu, kwa lengo la kuwawezesha watu walio na ulemavu (mikono) kuweza kutumia mouse bila kuwa na tatizo

INAYOHUSIANA  WhatsApp inaweza kuchezewa

Animouse inatumia WebCam ya Kompyuta yako na ‘Software’ ya kubashiri sura (Facial recognition) ili kuitafuta sura yako katika kufanya kazi

Uso

Mara tuu Animouse inapokupata, itapeleka msale wa mouse (cursor) sawa sawa na sehemu ambayo utakuwa ukipeleka kichwa chako katika kompyuta (kulia,kushoto,juu au chini)

Muhimu: Animouse ni program ambayo ni ya bure kabisaa! Na inapatikana katika njia ya wazi (Open source) hii ikiwa inamaanisha kwamba kama programa mwingine anataka kuiboresha au kufanya baadhi ya maboresho, anaruhusiwa. Animouse inafanya kazi kwenye kompyuta za Windows tuu.Animouse

go JINSI YA KUSHUSHA/KUPAKUA

Bofya Hapa Kuingia katika mtandao wa mouse hiyo na kisha click file la kudownload ambalo lina Zip yaani ‘Download Animouse Zip‘. Ukishamaliza shusha faili hilo fungua faili lako la zip, kisha tafuta App ya Animouse na baada ya hapo yatoe katika mfumo ambao mafaili hayo yapo (Extract). Na mwisho kabisa bofya App ya Animouse ili kuanza kuitumia.

INAYOHUSIANA  Bios Cube: Majivu ya marehemu kutumika kukuza mmea

animouse

here Angalia Video Kwa Ufupi Namna Animouse inayofanya kazi

Tuambie kama makala hii imekupa ujanja mwingine ambao ulikuwa haufahamu. Kumbuka Laptop yako ikiharibika kipanya(mouse) chake sio mwisho kuna njia nyingi za kufanya kama vile kununua mouse ya nje au hata kwa kutumia Animouse.

Tuandikie sehemu ya comment, umeipokea vipi makala hii. Endelea kutembelea mtandao wa TeknoKona

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply