Apple Kuja na iPhone Ndogo Bei Nafuu '#Uvumi' - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple Kuja na iPhone Ndogo Bei Nafuu ‘#Uvumi’

1
Sambaza

Kupitia moja ya chanzo cha kuaminika cha habari kuhusu kampuni ya Apple, inaonekana tujiandae na ujio wa iPhone ndogo hivi karibuni itakayofahamika kwa jina la iPhone 6c.

Kwa kipindi kirefu kuanzia kwa miaka ya Steve Jobs, kampuni ya Apple ilisemaka haioni umuhimu wa simu kubwa, yaani za zaidi ya inchi 4 – huku wakiziponda simu zenye kioo kikubwa enzi hizo kutoka makampuni kama ya Samsung. Lakini mabadiliko huwa yanatokea na kwa sasa kampuni hiyo tayari ilishaacha kutengeneza simu zenye umbo dogo baada na wao kuanza kutengeneza simu zenye umbo kubwa tuu.

Apple Kuja na iPhone Ndogo

Michoro ya kibunifu juu ya iPhone 6c

Ming-Chi Kuo – jamaa mwenye sifa kubwa katika kutoa habari mbalimbali zinazohusu kampuni ya Apple mapema zaidi na mwishoni zinatangazwa rasmi.

Data zinaonesha bado kuna soko kubwa za simu zenye maumbo madogo, kuna watu wengine hawapendi simu pana. Sababu nyingine kubwa ya uwepo wa soko ilo ni kwamba baadhi ya watu wanaviganja vidogo na hivyo ujio wa simu za iPhone kubwa umewafanya ata wapunguze upendo wao kwa simu za iPhone.

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Wamiliki/Viongozi wa kundi kuamua nani atume ujumbe

Bei ya simu hiyo itakayofahamika kwa jina la iPhone 6c itauzwa kati ya dola 400 hadi 500 za kimarekani, yaani kwenye Tsh 1,000,000 hivi. Kisifa inasemekana haitakuwa na tofauti sana na iPhone 6S bali itakuwa ndogo na itakosa vitu kama vile ‘fingerprint sensor’ na vitu vingine vidogo ambayo vitabakia kwenye matoleo ya iPhone kubwa tuu.

Apple Kuja na iPhone Ndogo

Michoro ya kibunifu ikionesha muonekano wa iPhone ndogo inayotegemewa kutangazwa rasmi na Apple

Soko la simu ndogo linasemakana bado lipo kubwa tuu. Zaidi ya asilimia 20% ya watumiaji simu nchini Marekani wanasema bado wanapendelea simu ndogo za inchi 4.

Taarifa ya ujio wa simu hii inasemekana kuwa ya ukweli kwa zaidi ya asilimia 80. Chanzo ni kutoka kwa jamaa anayeheshimika sana kwa kuwahi kutoa siri mbalimbali zinazohusu bidhaa za Apple mapema zaidi kabla ya taarifa rasmi kutoka kwa kampuni hiyo.

INAYOHUSIANA  Ondoa vitu kwenye Thumbnails kuongeza nafasi

Wengi bado wanaamini kama Apple wapo kwenye mpango huo wa kuleta iPhone ndogo basi wanaweza fanikiwa kimauzo pia, ingawa bado iPhone kubwa (inchi 5 na kuendelea) zitakuwa ndio zinazoongoza kimauzo na kifaida. Tutaendelea kufuatilia habari hizi na kaa tayari kupata taarifa zaidi.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Apple Kuja na iPhone Ndogo ya Bei Rahisi ‘#Uvumi’ | Teknolojia

Leave A Reply