Apps Kupitiwa na Google Kabla ya Kuingia Google Play

Apps Kupitiwa na Google Kabla ya Kuingia Google Play

0
Sambaza

Baada ya muda mrefu kupewa sifa mbaya ya kwamba soko la apps la Google Play ni moja ya soko lenye apps nyingi zilizo chini ya kiwango na zisizokuwa na sifa nzuri za kiusalama na za kiubunifu kampuni ya Google imeamua kuliangalia jambo hilo.

Kuanzia sasa ili app iingizwe na kuanza kupatikana katika soko hilo la apps lazima mtengenezaji yaani ‘Developer’ atume app yake kwenda kwenye kampuni hiyo. Timu yao itapitia na kuruhusu au kuwasiliana na mtengenezaji huyo na kumtaka afanye mabadiliko flani au kukataa kabisa kuweka app hiyo kwenye Google Play.

Google-Play-Store-logoMfumo huu umekuwa ukitumika kwa muda mrefu zaidi kwenye soko la apps la App Store linalopatikana kwenye iOS, inayotengenezwa na Apple kwenye vifaa kama iPhone, iPad na ata kompyuta za Macs. Mfumo huu umeipa sifa App Store ya kuwa soko lilokuwa na apps nzuri na zilizokwenye kiwango kikubwa zaidi.

INAYOHUSIANA  Youtube: Kipengele cha Dark Mode kwenye simu

Google wamewahaidi watengenezaji wa apps wasiwe na wasiwasi kufikiri ya kwamba mfumo huu utafanya apps zao zichelewe kuingia kwenye Google Play, amesema watajitaidi kuhakikisha ndani ya siku chache kama mbili tatu apps zao ziwe zimeingia Google Play. Hii ni kwa sababu ucheleweshwaji katika utaratibu huu ni jambo kubwa linalowauzi watengenezaji wengi wa apps kwenye iOS wanaotuma apps zao kwa kampuni ya Apple kwa ajili ya kupitiwa na kuingizwa kwenye AppStore. Inasemekana mara nyingi kwa Apple utaratibu huu unaweza kuchukua zaidi ya ata wiki mbili hadi App kuingizwa kwenye App Store.

Jambo jingine ambalo Google wamesema lipo katika kufanyiwa kazi na hivyo watengenezaji wapya na wa zamani wa apps wajiandae nalo ni suala la kuweka vigezo katika apps zao. Vigezo hivi ni pamoja na kuelezea makundi maalumu ya umri na sifa ambazo apps hizo zinaweza tumiwa. Hii ni kwa sababu kuna apps nyingine hazifai kutumiwa na watoto wadogo.

INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

Endelea kusoma TeknoKona, kumbuka kusambaza makala uzipendazo kuhakikisha tunaendelea kukua zaidi! 🙂 Kwa maswali na msaada usisite kutuandikia kwenda mhariri@teknokona.com

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply