Hizi ndio apps salama zaidi kwa kuchati – ripoti ya Amnesty International, 2016!

1
Sambaza

Hakuna mtumiaji wa simu janja duniani asiyetumia programu tumishi (apps) katika simu yake na hii ni kwa sababu tunahitaji programu tumishi ili kuweza kutumia simu zetu vizuri zaidi.

Katika taarifa zilizotoka hivi karibuni katika mitandao kama vile Telegram, Amnesty International zimetoa takwimu kuhusiana na programu tumishi zilizo na ulinzi zaidi kwa mwaka 2016. Lakini unaweza ukawa unajiuliza Programu tumishi ni nini?

Programu tumishi au apps kama wengi wetu tulizoea ni programu fulani unaweza kutumia kwenye simu au kompyuta katika kufanikisha jambo fulani.

Mfano wa apps ni Facebook Messenger, WhatsApp, Gmail, GDrive, n.k.

Orodha ya programu tumishi/apps zilizo na usalama zaidi kulingana na kampuni inayoimiliki/inayozimiliki

  • Facebook

Facebook inamiliki programu tumishi mbili; WhatsApp na Facebbok Messenger. WhatsApp ambayo hivi sasa inashikilia namba moja kwa kuwa app ambayo ina ulinzi wa kutosha; mazungumzo baaina ya mtu na mtu au mazunguzo ya kwenye group yanabaki kuwa kati yenu wawili.

WhatsApp na FB Messenger zote zinamilikwa na Facebook.

WhatsApp na FB Messenger zote zinamilikwa na Facebook.

Facebook Messenger si salama sana kwa sababu yenyewe haina feature ijulikanayo kama end-to-end encryption. Apps hizi 2 kwa ujumla zina watumiaji zaidi ya bil. 2. 

Ilipata kura 73/100

  • Apple

Kampuni hii yenye kumiliki iMessage na Facetime yenyewe imeshika nafasi ya pili katiaka orodha ya apps zenye uinzi wa kuaminika kwani apps hizo 2 haziwezi kuonyesha taarifa kwa mtu asiyehusika (iwapo app ikidukuliwa) hakuna atakayeweza kuelewa isipokuwa Apple wenyewe. Hata hivyo apps hizi zimetakiwa kuwaeleza watumiaji wote ni muda taarifa zao zinakuwa salama na ni wakati hazipo salama mathalani iwa mtu atatuma ujumbe kwenda kwa mtu asiyetumia iPhone.

SOMA PIA:  Google yaruhusu mtu kuweza kutengeneza "Google Maps" zake na kuzisambaza

Ilipata kura 67/100

Apple wameweka wazi kuwa wenyewe watatoa taarifa za mtu/watu iwapo serikali ikizihitaji

Apple wameweka wazi kuwa wenyewe watatoa.

  • Telegram

Telgram in app ambayo ilikuwa ya kwanza kuwezesha watu kutuma nyaraka katika mfumo wa “.doc” kabla ya app nyingine yoyote kuiga kitu hicho. Cha kushangaza ni kwamba Telegram ile feature ya ‘end-to-end encryption’ sio ya papo kwa papo (default); huwezi kujua ni wakati gani taarifa zalo zipo salama.

Ilipata kura 67/100

Telegram inawatumiaji wa mara kwa mara takribani 100 milioni kila mwezi

Telegram inawatumiaji wa mara kwa mara takribani 100 milioni kila mwezi

  • Google

Google ambao ni wamiliki wa programu tumishi Allo, Duo na Hangouts. Ukiwa na Allo app basi mawasilisno yataabaki kuwa baina yenu mnaowasiliana tu huku kwenye Duo ni chagua lako kukubali end-to-end encryption au kukataa. Hangouts haina end-to-end encryption kwahiyo si salamasana kwani taarifa zako hazijafichwa.

SOMA PIA:  Instagram Yaja Na 'Sticker' Kama Snapchat!

Ilipata kura 53/100

alloduo-hangouts

Google hutoa taarifa za mtu/watu iwapo serikali ikizihitaji.

  • Line

Line iliyo maarufu sana nchini Japan, Indonesia, Thailand na Taiwan yenye watumiaji zaidi ya 200 milioni kila siku. Hii ni programu tumishi maarufu sana katika nchi hizo kwa sababu usalama wa taarifa za watumiaji wake unatunzwa bila ya mtumiaji kuwaza iwapo taarifa zake zipo salama au la! Na haitoi taarifa kwa mtu yeyote au kwa serikali iwapo zikihitajika.

Ilipata kura 47/100

App ya Line ni app ya kuiamini sana ingawa si maarufu katika nchi nyingi.

App ya Line ni app ya kuiamini sana ingawa si maarufu katika nchi nyingi.

  • Viber

Viber ni app inayofanana sana na Sype; unaweza ukatuma msg, ukapiga simu kwa njia ya video au kawaida kwa kutumia intaneti, ukapiga simu kwa mtu yoyote kwa kulipia kiasi fulani cha pesa. Ina watumiaji takribani 750 millioni na zaidi ya watumiaji 200 milioni kwa siku. Usalama wa taarifa za watumiaji wake unatunzwa bila ya mtumiaji kuwaza iwapo taarifa zake zipo salama au la!

SOMA PIA:  Kampuni ya Uber yapata Mkurugenzi Mtendaji mpya

Ilipata kura 47/100

Viber hawatoi taarifa za kueleza ni kwa kiasi gani taarifa za watumiaji wa app hiyo zipo salama.

Viber hawatoi taarifa za kueleza ni kwa kiasi gani taarifa za watumiaji wa app hiyo zipo salama.

Apps nyinginezo

Kakao ni app inayomilikiwa na kampuni moja nchini Korea Kusini na ina watumiaji hai 49 milioni kila mwezi. Skype ambayo ipo chini ya Microsoft tangu mwaka 2011 ina watumiaji zaidi ya milioni 300. Snapchat nao hawapo mbali kwani wana watumiaji milioni 100 kwa siku ingawa hawajaweka ulinzi madhubuti katika kutunza taarifa za wateja wake.

BlackBerry inafunga orodha kwa app yake ya BBM yenye watumiaji takribani 100 milioni na huduma ya end-to-end encryption ni kwa kulipia tu (sio bure).

Ni wakati wako sasa wa kuchagua app gani ya kuendelea kutumia na ni ipi ya kuachana nayo. Una mtazamo gani kuhusiana na hili. Niandikie katika sehemu ya maoni hapo chini.

Vyanzo: Amnesty International, Telegraph

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com