Baada ya Huawei Mate 10 kutoka sasa ni zamu ya Huawei Mate 10 Pro - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Baada ya Huawei Mate 10 kutoka sasa ni zamu ya Huawei Mate 10 Pro

0
Sambaza

Karibu miezi miwili sasa tangu Huawei Mate 10 kuanza kupatikana nchi nyingi duniani baada ya kuzinduliwa mwezi Agosti mwishoni tayari toleo jipya kutoka familia ya Huawei Mate lipo njiani kutoka.

Huawei ni kampuni iliyo katika nafasi ya tatu (kwa mujibu wa takwimu za karibuni sana) kati ya zile kampuni zinazoongoza katika utengenezaji wa simu janja. Huawei Mate 10 Pro imetengenezwa kwa lengo la kushindana vikali na simu janja kutoka kwa mahasimu wakubwa wa Huawei, yaaani Apple na Samsung.

Huawei Mate 10 Pro imewekewa nguvu zaidi katika maeneno makuu matatu; ukubwa wa kioo, uwezo wa betri (kutunza chaji kwa muda mrefu) na kuweza kuotea mahali unapotaka kubonyeza (Artificial Intelligence).

Undani wa sifa zilizopo kwenye toleo jipya la simu janja Huawei Mate 10 Pro.

Kabla ya mengine yote ni vyema ukafahamu muundo wa Huawei Mate 10 Pro. Simu hii kwa nyuma ipo katika follow mfumo wa mkunjo (curved) halafu pembezoni ina malighafi ya chuma ambayo inaifanya simu hii hata ikianguka iwe ngumu kudhurika.

Muonekano wa nyuma wa Huawei Mate 10 Pro; simu ambayo inalenga kueta ushindani thabiti dhidi ya Apple na Samsung.

watch Kioo na Prosesa. Kioo cha kwenye Huawei Mate 10 Pro kina ukubwa wa inchi 6 na kioo hicho kinatumia teknolojia ya source link OLED katika kuhakikisha kuwa chochote kinachoonekana katika uso wa simu basi kinaonekana katika muonekano ang’avu wa hali ya juu. Prosesa iliyopo kwenye simu hi toleo la hivi sasa, Kirin 970 inayoifanya simu hii kuwa na kasi mara 25 zaidi na werevu (AI) mara 50 zaidi.

INAYOHUSIANA  Bakhresa aanzisha kampuni ya mawasiliano ya simu-Azam Telecom

Kamera na betri. Huawei wameipa ubora kwa kutosha toleo hili jipya kutoka kwenye familia ya Huawei Mate. Kama ilivyo katika simu nyingi za karibuni, simu hii ina kamera mbili za nyuma zenye MP 20 pamoja na sensa za MP 12; sensa zilizopo kwenye kamera ndio zenye jukumu la kupiga picha.

Betri yake ina nguvu kiasi cha 4000mhA huku simu hiyo ikiwa na ile tekmolojia ya kuchaji simu haraka ambapo kuchaji kutoka 0%-58% ndani ya dakika 30 tu!

Kamera yake kwa kutumia sensa itaweza kutumia teknolojia ya AI na hivyo kujua wapi unataka kwenda kwenye simu hiyo. Teknolojia ya alama ya kidole haijasahaulika kwenye simu hii.

RAM na diski ujazo. Katika kuboresha katika kila simu janja zinazotoka imeonekana makampuni mengi yameanza kuachana na kuweka uwezo wa GB 4 kushuka chini na nyingi ambazo zimetoka/zinatoka zinakuja na RAM GB 6 kama ilivyo kwenye Huawei Mate 10 Pro. Diski ujazo wa simu ni GB 128 na haina sehemu ya kuweka ujazo wa ziada (micro SD card).

Bei na upatikanaji. Gharama ya toleo hili jipya kutoka familia ya Huawei Mate ni karibu $945|Tsh. 2,125,305 ambapo simu hii itaanza kupatikana katikati ya mwezi Novemba kwa Ufaransa, Itali, Ujerumani, Thailand, na nyinginezo.

INAYOHUSIANA  Uber waanza na India kutoa toleo dogo kabisa la programu tumishi

Sifa nyinginezo za Huawei Mate 10 Pro.

  •  Huawei Mate 10 Pro ina teknolojia ya USB Type-C ambayo unaweza ukaunganisha kioo cha nje (monitor) na hivyo ikatumika kama kompyuta. Unaweza pia ukaungamisha ‘kipanya’ na keyboard kwa kutumia Bluetooth na hivyo kuifanya kuwa kompyuta kamili.
  • Haiingii maji (waterproof) lakini pia Huawei wameamua kutoweka sehemu ya kuchomekea spika za masikioni.
  • Inakuwa simu ya pili kuja na toleo jipya la programu endeshaji ya Android, Android 8 (Oreo) baada ya mtangulizi wake (Huawei Mate 10) nayo kuwa na programu endeshi hiyo hiyo.
  • Inakuja katika rangi nne; kahawia, rangi ya maziwa, zambarau ya dhahabu na bluu isiyokolea na inakuja na uwezo wa kuweka laini mbili za simu.
INAYOHUSIANA  Samsung kuzindua memori kadi ya 512GB

Simu hii inatazamiwa kuleta ushindani mkali dhidi ya wapinzani wa kubwa wa Huawei kutokana na kwamba simu hii ina teknolojia ya Artificial Intelligence (AI) iliyowekwa ndani kwa ndani.

Vyanzo: The guardian, Android Authority, Huawei, Techradar

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.