Bodi ya Filamu Kenya yasema NETFLIX lazima ifuate sheria

0
Sambaza

Bodi ya uchambuzi wa filamu Kenya (KFCB)  imesema kwamba ni lazima huduma ya NETFLIX ifuate sheria za filamu za Kenya na kama watakiuka sheria hizo basi watafungiwa kurusha huduma zao.

KFCB inasema kwamba imegundua kwamba NETFLIX ina filamu na tamthilia ambazo hazifuati sheria zilizowekwa kutawala sekta ya filamu, KFCB imesema inategemea kukutana na NETFLIX siku ya Jumatatu na kisha kujadili sera za Kenya katika filamu za nje.

Afisa mtendaji mkuu wa KFCB Ezekiel Mutua amesema kwamba watatumia sheria ya filamu na Maigizo ambayo inashughurika na kusimamia filamu, pia aliongeza sheria ya mawasiliano na habari inawapa mamlaka ya kufungia  ama kuweka vikwazo filamu zinazorushwa na vituo kwa mtandao ama kwa njia ya kawaida.

Kenya netflix

Logo ya Netflix.

Katika kauli yake  kwa gazeti la Business Daily  Mutua amesema kwamba wangeweza kuwafungia NETFLIX kwa kuleta bidhaa bila ya wao KFCB kuzichambua, hata hivyo amesema kwa kuwa hawataki kuwaogopesha wawekezaji wa kigeni basi wataenda na kuwaona NETFLIX na kuwaambia viwango vya filamu za Kenya.

NETFLIX imekuwa ni gumzo katika viunga vya Nairobi tangu ilipotangazwa kuwa huduma hii itaanza pia kupatikana Kenya, kwa vyovyote vile italeta taflani endapo kwa namna yeyote ile KFCB itaifungia huduma hii. Ukweli ni kwamba kisheria KFCB wanayo haki ya kufungia huduma ya NETFLIX ila je ni kweli kwamba kila filamu inayorushwa inakidhi vigezo vya bodi hii?

SOMA PIA:  Google yakiri kuwafuatilia watumiaji wa simu janja za Android

Kipindi cha nyuma KFCB ilishwa wahi kufungia baadhi ya filamu kuoneshwa,kuuzwa ama kusambazwa ndani ya Kenya kutokana na kukiuka vigezo, baadhi ya filamu zilizowahi kufungiwa ni pamoja na “The Wolf of Wallstreet na The shades of Grey.

 
Tuambie kwenye sehemu yetu ya maoni (comments) nini ni mtazamo wako juu ya vigezo vinavyowekwa na bodi zetu za filamu.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com