Dondoo za Ulinzi na Usalama wa Pesa na Huduma za Kibenki ktk Simu Yako

0
Sambaza

Tayari hadi TCRA wameshazungumza kuhusu hatari za wizi na udanganyifu unaoweza kufanyika kupitia simu za mkononi, hasa hasa katika kuwaibia watu pesa zao kupitia ufanyaji wa malipo kupitia simu za mkononi. Leo TeknoKona tutakupa dondoo kadhaa za kukusaidia kuendelea kuwa salama katika utumiaji wako wa malipo kutumia huduma za mitandao ya simu au benki yao kwa kutumia simu yako.

mawasiliano-tcra-tanzania

Dondoo hizi zinakusaidia pia kama unatumia app kutoka benki yako kama vile CRDB, NMB, Barclays na zinginezo

1. Hakikisha unaweka nenosiri (password) katika simu yako

Hii ni moja ya hatua muhimu zaidi katika kuhakikisha pesa zako zilizopo kwenye huduma ya kibenki ya simu au akaunti yako ya benki kupitia app inakuwa salama. Kwani kama mtu hafahamu password ya simu yako ata kama anajua password ya huduma ya Tigo pesa, M-Pesa au Airtel Money yako bado hataweza kufanya lolote kuhusu akaunti yako.

SOMA PIA:  MiniTool Power Data Recovery: Programu ya kuokoa data zilizofutwa au kupotea

Kama inakubidi kumuhusisha mtu mwingine unayemuamini sana basi ni huyo tuu ndio hafahamu, ila kumbuka pia mara nyingi inaripotiwa wanaowaibiwa wengine pesa inakuwaga ni wale wanaoaminika zaidi.

Pia kama unaweka pesa nyingi kwenye huduma ya pesa za mitandao ya simu hakikisha umeweka password/Lock ya kadi ya simu pia. Hili unaweza kulifanya ukienda kwenye mipangilia(settings) ya ‘Sim Card’ katika simu yako.

2. Futa SMS za huduma ya benki mara kwa mara

Kweli kabisa, sio unapokea meseji zinazosema umebakiwa na kiasi gani kwenye akaunti yako na unaziacha tuu huku simu yako ikiwa haina uangalizi mzuri. Kwani kama huwa unaweka pesa nyingi iwe ni benki au kwenye huduma za kipesa za simu basi kama mtu akichungulia na hakakuta una mapesa kibao inaweza wachochea kutaka kukuibia.

3. Ukiibiwa simu tuu hakikisha unatoa ripoti mara moja

Hapa fikiria kama hauna password katika simu yako na ghafla simu hiyo imepotea, hakikisha unatoa ripoti mara moja polisi na ata kwa mtoa huduma wako rasmi (mtandao wa simu) ili waweze kuifunga akaunti yako ya laini.

SOMA PIA:  Namna ya kuweka Play Store katika simu zenye mfumo wa kichina

4. Hii itakusaidia kuepuka mambo kadhaa;

Mtu kufanya miamala ya kipesa kutoka kwenye akaunti yako, yaani kukuibia pesa hasa kama atakuwa amefanikiwa kuotea au kuwa na password yako ya huduma za fedha.
Mtu kutumia akaunti/laini yako kwa ajili ya kufanya uharifu ambao unaweza ukajikuta unahusishwa nao bila wewe kuwa na ushiriki wowote katika jambo ilo.

5. Mara zote usikubari mtu mwingine akuombe taarifa zako za siri/muhimu kupitia mazungumzo ya simu

Hapa tunamaanisha ata kama mtu akikupigia kwa simu na kujitambulisha kama ni mtoa huduma kutoka mtandao wa simu unaotumia au benki unayotumia na akataka umpatie taarifa zako muhimu kama vile PIN/Password ya akaunti yako usikubali kabisa. Fika katika ofisi husika na kutaka maelekezo zaidi.

SOMA PIA:  Firefox Send: Mozilla waja na huduma ya kutuma mafaili kwa usiri

6. Epuka Kutuma Pesa kwa Ndugu/Jamaa unayemfahamu akikuomba msaada kwa ujumbe mfupi/SMS

PIGA SIMU KWANZA! Ndio, inawezekana ni mtu mwingine kabisa ndio anasimu ya huyo ndugu yako na akawa anafahamu password ya huyo ndugu na hivyo ukituma pesa tuu mtu huyo asiyehusika anaweza kwenda na kutoa pesa hizo mara moja. UTAKUWA UMEINGIZWA MJINI, ata kama upo kijijini na aliyefanya hayo yupo kijiji hicho hicho. 🙂 Ndugu au rafiki akiomba msaada wa pesa, tafadhali piga simu na kuhakikisha ya kwamba unamtumia pesa mtu sahihi.

Je, ni kosa gani umekuwa unalifanya sana kati ya haya tuliyoyataja? Pia tungependa kusikia kutoka kwako, wewe unafanya nini kuhakikisha kunakuwa na usalama wa huduma zako za kibenki katika simu yako?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com