Kama bado ulikuwa hujaliona gemu la chess ambalo lipo katika app ya Facebook ya Messenger basi Teknokona inayofuraha kubwa leo kukuibia siri hii kutoka kwa watengenezaji wa app hii.
Watengenezaji wa Messenger kwa siri wameweka gemu la Chess katika app hii na mtu unaweza kulicheza ukiwa sehemu ya kuandika ujumbe, kabla hujaacha kusoma makala hii na kukimbilia kujaribu hii kitu naomba nikujulishe kwamba sio tuu ujuzi wa kucheza chess unaohitajika hapa bali pia utahitaji kuzijua command ambazo zinatumika kucheza mchezo huu.
Kuanzisha gemu hili unatakiwa kufungua sehemu ya kuandika ujumbe katika app yako na kisha andika command ya kuanzisha gemu hili ambayo ni “@fbchess play” (bila ya alama za kunukuu) hii itakufungulia letea gemu hilo la Chess kwa ajili ya kucheza na mpinzani wako ambaye ni mtumiaji ambaye ulikuwa umemchagua kumuandikia ujumbe.
Kama unataka kuufaidi mchezo huu basi inakupasa ujifunze sheria pamoja na ufundi unaohitajika, maana hii inaweza kuwa njia nyingine ya kupoteza muda na rafiki yako wa karibu ama mpenzi wako.
Kucheza toleo hili la Chess kwanza ni lazima uwe unajua majina ya kete za mchezo huu, baada ya hapo utahitaji kujua vifupi vya majina haya ambavyo ndio vinatumika katika commands za kusogeza kete. Kinatumika badala ya King Q = queen, B = bishop, N=knight, R = rook na P = pawn.
Chess inakuja ikiwa na namba katika mistari ya usawa (holizontal) na huku herufi a, b, c, d, e, f, g, h zikiwa zimeandikwa katika mistari ya wima (vertical) hivyo kama unataka kuhamisha tuseme Pawn kwenda katika kibox mbele ambacho kiko katika mstari wa wima wa d na mstari wa usawa wa 3 basi utaandika ‘@fbchess Pd3‘ (bila ya alama za nukuu) hii itaifanya kete yako ya pawn ihame hadi katika box husika.
Facebook wamekuwa wakijaribu kila linalowezekana kuifanya messenger iwe ni app inayopendwa na kutumiwa na watu wengi zaidi, utakumbuka kwamba ili kutma ujumbe katika simu basi utahitaji kuipakua app hii hivyo hili linaonekana kama ni moja ya jaribio la kuhaikikisha kwamba watu wanaipenda na kuitumia zaidi app hii.
No Comment! Be the first one.