Fahamu Matoleo Rasmi ya Windows 10

0
Sambaza

Kama ni msomaji wa siku zote wa mtandao wako wa TeknoKonaDotCom basi utakuwa tayari unafahamu ya kwamba muda si mrefu toleo jipya la Windows 10 linaingia sokoni, na sasa Microsoft kupitia blogu yao rasmi wameeleza rasmi matoleo tofauti ya Windows 10  kwa ajili ya mahitaji na vifaa tofauti.

Windows-10-simu-kompyutaPia kupitia taarifu hiyo wameelezea baadhi ya sifa zitakazohitajika kwa watumiaji watakaoweza kupata chagua la kufanya msasisho (update) wa bure wa kuweka Windows 10 kwenye kompyuta au vifaa vyao vingine vinavyotumia Windows.

>Windows 10 Home; Hili ni toleo la kawaida kwa ajili ya watumiaji ya aina zote. Toleo hili ndilo litakuwa linakuja pia kwenye kompyuta na laptop mpya zinatakaziuzwa madukani kwa ajili ya watu wote.

>Windows 10 Mobile; Hili ni toleo spesheli kwa ajili ya simu na tableti.  Toleo hili litakuwa na karibia apps zote muhimu zinazokuja na toleo linalotumika katika kompyuta ila pia apps/programu hizo zitaweza kutumika kwa mguso (touch). Baadhi ya simu/tableti zitakazokuwa na uwezo mkubwa zaidi zitapata toleo la Windows 10 Mobile lenye teknolojia ya Microsoft Continuum.

SOMA PIA:  SanDisk imeleta memori kadi ya ukubwa wa GB 400

Je teknolojia ya Continuum ina nini hasa?

  • Simu/tableti yenye teknolojia hii ikiunganishwa na kifaa cha mtazamo (Display) kama vile TV basi utaweza kuona na kufanya kazi zingenezo kutumia kioo hiko, na si hapo tuu bali programu endeshaji hiyo itabadili muonekano kutoka ule wa kisimu na kujibadili kulingana na ‘display’ hiyo.
  • Pia kama utaunganisha Kipanya (mouse) na Kibodi katika kifaa kama tableti yenye toleo hili la Windows basi vifaa hivi vitaweza kufanya kazi katika ubora mkubwa tuu.

>Windows 10 Pro; Toleo la Windows Pro ambalo huwa linalenga utumiaji wa kikazi kubwa zaidi. Mara nyingi tofauti kubwa kati ya toleo la Windows la Pro na lile la kawaida (Home) linakuwaga linajumuisha sifa kama vile uwezo mkubwa zaidi wa kuhimili RAM za GB kubwa zaidi, pia na uwezo wa utumiaji wa teknolojia zingine nyingi za kikazi zaidi kwa ajili ya maofisi n.k

SOMA PIA:  Google na Microsoft waungana katika vita dhidi ya mitandao ya mafaili ya wizi

Hayo ndiyo matoleo makubwa, ila pia kuna matoleo mengine;

>Windows 10 Enterprises; Hii ni toleo la Windows 10 Pro lililoongezewa teknolojia spesheli kwa ajili ya kompyuta zinazotumika katika masuala ya data kubwa makazini.

>Windows 10 Education; Hili ni toleo linalotumia teknolojia ya Windows 10 Enterprises ila ikiwa imebuniwa na kuboreshwa kwa ajili ya mahitaji ya kielimu – yaani wafanyakazi mashuleni, walimu, pia na wanafunzi.

>Windows 10 Mobile Enterprise  ni toleo spesheli litalokuwa linatumika katika vifaa vidogo vya kijanja kama vile simu spesheli kwa matumizi ya kiofisi na mashine za ATM (Ila  mfumo mama wa ATM unaweza ukawa chini ya programu endeshaji ya Windows 10 Enterprise).

>Windows 10 IoT Core; Ushawahi kusikia kitu kinaitwa ‘Internet of Things’? Hivi ni vifaa vidogo vinavyotumika katika matumizi ya kawaida ya kila siku ila vikisaidiwa na teknolojia inayotumia intaneti… Mfano inaweza ikawa kwa kamera janja.

SOMA PIA:  Nova Launcher yapakuliwa mara milioni 50 mpaka sasa

Je sasisho (update) za bure kwenda Windows 10 zitatolewa kupitia intaneti kwa matoleo gani ya Windows yanayotumika sasa?

Kama kompyuta yako inatumia toleo la Windows 7 au 8 basi kuwa tayari kupata uwezo wa kusasisha (update) kwenda Windows 10 bure kabisa katika kipindi cha mwaka mmoja kupitia intaneti. Pia kwa simu zinazotumia toleo la Windows Phone 8.1 zitaweza kupata sasisho hilo bure kabisa.

Soma Pia;

Asante kwa kutembelea TeknoKona, kumbuka kusambaza makala kwa marafiki kupitia Twitter, Facebook, WhatsApp na njia nyingine yeyote. Asante sana!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com