Sasa Fahamu Ujumbe Ukisomwa Katika WhatsApp

0
Sambaza

whatsapp_tanzaniaKwa muda mrefu watu wengi walikuwa wanachanganya uwepo wa ‘tick’, alama ya vyema/kupata ya kuwa inaashiria ujumbe kusomwa kwa mtu aliyeupokea. SI KWELI! Ukweli ni kwamba muda wote huo alama ya vyema moja kwenye WhatsApp imekuwa ikiashiria ujumbe umefikia mitambo ya WhatsApp (servers), na alama mbili za vyema zinaashiria ujumbe umepokelewa kwenye simu ya uliyemtumia na si kwamba ujumbe umesomwa kama vile wengi walikuwa wakifikiria.

Lakini sasa WhatsApp iliyonunuliwa na Facebook kwa mabilioni ya dolali itakufahamisha pale ujumbe usika utakaposomwa kupitia kubadilika kwa rangi wa alama hizo mbili za vyema kwenda rangi ya bluu.

WhatsApp_Tanzania

Kumbuka pia unaweza kubofya mara mbili ujumbe ulioutuma kuweza kuona taarifa zaidi kuhusu muda husika ambao ujumbe huo ulifika na kusomwa.

SOMA PIA:  #Maujanja - Tatua tatizo la kushindwa kupakua apps kutoka Google Play Store - Error 505

Watu wengi wamekasirikia uamuzi huu wakidai mambo mengine yanatakiwa kubakia kuwa siri….hii ni kwamba wengine wanapenda kuwa na uhuru wa kupotezea ujumbe wa mtu bila kuathiri uhusiano kwani wanaweza dai kwamba hawakuuona ujumbe husika, sasa kwa hili la kuonesha taarifa ya kwamba ujumbe umesomwa utaleta tabu kidogo….

Kazi ipo, je wewe umefuruhishwa na uamuzi huu?

Kumbuka unaweza kusoma habari na maujanja mbalimbali yahusuyo WhatsApp kupitia hapa ->http://teknokona.com/?s=whatsapp

(Picha kwa hisani ya TheNextWeb)

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com