Fununu za Samsung Galaxy S6

Fununu za Samsung Galaxy S6 – Fahamu nini Kinakuja

0
Sambaza

Wengi wanasubiria kwa hamu kufahamu Samsung wataleta nini cha utofauti katika toleo lao lijalo la simu za familia ya ‘Galaxy S’. Yaani Samsung Galaxy S6.

Hadi sasa tayari mambo kadhaa yameanza kujulikana, (kumbuka kuna ambayo yanaweza kuwa tofauti) nayo ni haya;

Muonekano wa kioo unaonekana umefunika hadi kona za mwisho wa simu kwa upande wa mbele

go here Muonekano wa kioo unaonekana umefunika hadi kona za mwisho wa simu kwa upande wa mbele

  • see url Inawezekana mfuniko wake wa nyuma ukawa wa madini ya chuma na si plastic kama matoleo yaliyopita.
  • Kuna uwezekano kukawa na matoleo mawili ya Galaxy S6. Moja ya muonekano wa kawaida na nyingine yenye umbo la mpindo (curved).
galaxy-s6

Picha kama hii kutoka Samsung ndiyo inayoleta wazo la kuwa na teknolojia mpindo (curved) katika Galaxy S6

 

  • Inasemekana kwenye Galaxy S6 Smasung wamepunguza ujazo wa Apps nyingi zisizokuwa za ulazima kutoka kwao kitu ambacho kilikuwa kinalalamikiwa sana. Hivyo tegemea kutoona apps kama vile ChatOn, Samsung Hub, My Galaxy, n.k
INAYOHUSIANA  Vodacom na wizi wa fedha mtandaoni

SIFA ZINGINEZO

  • Kioo cha inchi 5.2 au 5.3
  • Kamera ya nyuma – Mega Pixel 20! (Kwa kiwango hichi picha zitakuwa za kiwango kikubwa sana.
  • Betri ya 2600mAh (Si kiwango kikubwa)
  • Kuna vyanzoi vingi vinasema itakuwa na RAM ya GB 4
  • Kutakuwa na toleo lenye diski uhifadhi wa GB 32,64 na 128
  • Kuna uwezekano mkubwa ikaja na toleo la Android Lollipop (Android 5)

Utambulisho rasmi kutoka Samsung wa simu hii unategemea kufanyika mwezi ujao (Wa tatu), endelea kusoma TeknoKona.Com na tutakuelezea mambo yatakavyokuwa!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply