Gemu la Snake (Nyoka) Linakuja Kwenye Simu Janja

0
Sambaza

nokia-snake-gemuKaa Tayari Kucheza Lile Gemu la Enzi zilee! Kama mara yako ya kwanza kumiliki simu ilikuwa katika ile miaka ya elfu mbili mwanzoni, na wengine ata miaka ya 90 mwishoni basi utakuwa unafahamu kulikuwa na gemu lililokuwa maarufu sana. Gemu hilo halikuwa na mbwembwe nyingi sana, wala halikuwa la rangi pia.

Gemu hilo maarufu lilikuwa linaitwa Snake, yaani nyoka na lilikuwa linapatikana katika karibia simu zote za Nokia za kipindi hicho. Umelikumbuka?

SOMA PIA:  TV kwenye chumba cha mtoto/watoto wako humsababishia kuongezeka uzito #Utafiti

Gemu la Snake linahusisha mchezaji kuanza na nyoka mdogo ambaye ukuaji wake inambidi mchezaji ale vidoti vidogo vidogo vinavyojitokeza na kupotea kila baada ya muda. Kila anavyozidi kuwa mrefu na ndivyo kasi ya mchezo unaongezeka, na hautakiwi kumgogesha dhidi ya mwili wake mwenyewe, ukifanya hivyo gemu linaisha na itakubidi uanze upya.

airtel tanzania bando

Kwenye app hii utaweza kuchagua haina mbalimbali za muonekano na mambo mengine yahusuyo jinsi ya kucheza

Kwenye app hii utaweza kuchagua haina mbalimbali za muonekano na mambo mengine yahusuyo jinsi ya kucheza

Kuna kampuni imeshatangaza ujio mpya wa gemu ilo kwenye simu janja zinazotumia programu endeshaji za Android, Windows na za iOS. Kampuni hiyo, Rumilus Design, imesema app hiyo itaweza kupakuliwa bure kabisa na jina rasmi la gemu hilo litakuwa Snake Rewind.

SOMA PIA:  Memoji: App ya kuzifanya picha zako kuwa emoji.

Gemu ilo litaanza kupatikana tarehe 14 mwezi wa huu wa tano na wamesema ingawa wazo la gemu hilo ni kama lile la zamani bado wameweka vitu mbalimbali vya kisasa katika kulifanya lipendeze zaidi.

Gemu hili lilikuwa ni moja app maarufu sana kwa kipindi cha miaka ya nyuma enzi za utawala wa Nokia katika somo la simu

Gemu hili lilikuwa ni moja app maarufu sana kwa kipindi cha miaka ya nyuma enzi za utawala wa Nokia katika somo la simu

Je utataka kulishusha gemu hili kwenye simu/tableti yako likija? Endelea kutembelea TeknoKona na tutakutaarifa likiingia rasmi katika masoko ya apps.

SOMA PIA:  Facebook kufundishwa kama kipengele katika somo la Kiingereza nchini India

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com