Gmail Waleta Uwezo Wa Kurudisha Barua Pepe Mara Tuu Baada ya Kubofya Kutuma Kimakosa!

0
Sambaza

Mtandao wa barua pepe unaomilikiwa na kampuni ya Google wa Gmail umeleta rasmi uwezo wa mtu kurudisha barua pepe ambayo alikwisha bofya alama ya kuiruhusu kwenda, yaani ‘Send’.

Uwezo huu ulikuwepo kwa miaka kadhaa kwa watu wachache ambao iliwabidi wapitie eneo la Google Labs kuweza kuuwezesha.

Kama utakuwa umekosea barua pepe ya kwenda kwa rafiki ukamtumia bosi wako n.k basi uwezo huu utaweza kukusaidia sana kuepuka majanga ya namna hii.

SOMA PIA:  Instagram yazidi kuiiga Snapchat, yaleta face filters na Hashtags

Kuwezesha chaguo (setting) hii ingia kwenye mtandao wa Gmail na kisha nenda eneo la ‘Setting’ la barua pepe yako.

Ingia kwenye barua pepe ya Gmail kisha nenda eneo la Settings

Ingia kwenye barua pepe ya Gmail kisha nenda eneo la Settings

Bofya tiki eneo la ‘Enable Undo Send’ kisha chagua muda wa kuchelewa kwa ujumbe kutumw (muda upo ktk sekunde).

Bofya tiki eneo la 'Enable Undo Send' kisha chaguo muda wa kuchelewa kwa ujumbe kutumwa

Bofya tiki eneo la ‘Enable Undo Send’ kisha chagua muda wa kuchelewa kwa ujumbe kutumwa

Hii itakuwa ni habari njema kwa wote ambao huwa wanaandika barua pepe zao wakiwa katika haraka sana. Je, ushawahi kukosea katika utumaji wa barua pepe? Je unadhani uwezo huu ni muhimu sana?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com