HP yatoa kompyuta/tabiti ya kwanza ulimwenguni ambayo ni Workstation - TeknoKona Teknolojia Tanzania

HP yatoa kompyuta/tabiti ya kwanza ulimwenguni ambayo ni Workstation

1
Sambaza

Hewlett Packard (HP) kampuni ambayo imekuwa kwenye biashara ya vifaa vya teknolojia kwa miongo kadhaa sasa na kutokea kupendwa kutokana na bidhaa zake kuwa na imara pamoja na uwezo wa kuhimili mambo mbalimbali yanayoweza kuharibu bidhaa fulani kutoka HP.

HP ZBook X2 ni kompyuta mpakato/tabiti ambayo imekuwa kompyuta ya kwanza kuwa kwenye kundi la http://sessiontapes.com/tag/video/ “kompyuta zenye uwezo wa hali ya juu sana (workstation)” kutokana na uwezo wa komyuta hiyo. Kompyuta hii ina sifa lukuki mfano keyboard inayochomoka na kuweza kutumika bila kuwa imeunganishwa na kompyuta/tabiti, unaweza ukatumia kalamu ya kidigiti, kuweza kuwekwa katika nyuza 160 na bado kuotumika kama kompyuta inayoonyesha keyboard nzima.

HP ZBook X2

Tabiti ambayo keyboard yake inaweza kutumika hata bila kuwa imeunganishwa na kompyuta kwa pamoja-moja ya sifa za teknolojia ya Bluetooth.

Uchambuzi wa sifa za HP ZBook X2 (Tabiti ambayo ni workstation).

Mpaka hivi wa leo http://preaknessstakeswagering.com/tag/tiaras-tango/ tumeshaona tabiti (tablet) nyingi sana lakini hakuna hata moja iliyofanikiwa kuwekwa katika kundi la kuwa workstation kutokana na kwamba kama kompyuta ni workstation basi ujue uwezo wake si mchezo. HP ZBook X2 ina sifa zifuatazo:-

buy pfizer viagra online usa Prosesa. Moja ya kiungo muhimu sana kwenye kompyuta yoyote ni uwezo wa prosesa na basi kwanini HP ZBook X2 imwekwa kwenye kundi la kuwa workstation? Jibu ni quad-core Intel Core i7 au i5 prosesa yenye kasi ya mpaka 4.2GHz na ina sehemu ya kuweka NVIDIA Quadro graphics kadi. Ina feni mbili kwa ajili ya kupooza prosesa.

Kioo na ubora wa pichaHPZBook X2 ina kioo chenye ukubwa wa inchi 14 (3,840×2,160 pixels) ambacho ni kioo cha mguso na ukipenda uweza ukatumia kalamu ya kidigitali kubonyeza kwenye kioo. Picha zake ni za kiwango cha 4K.

HP ZBook X2 ina kamera mbili, ile ya nyuma ina MP 8 na ile ya mbele ina MP 720. Uzuri wa tabiti hii ni kwamba kalamu yake ya kidigiti haihitaji kuchajiwa; yaani unatumia tu bila hofu kwamba itaishiwa na chaji.

RAM na diski ujazo. Hapa HP wajafanya mzaha na kuthibitisha kuwa tabiti hiyo ni sahihi kabisa kuwa kwenye kundi la workstation, inakuja na RAM GB 32 huku diski ujazo ukianzia 128GB, 256GB, 512GB na 1TB.

Betri. Sifa nyingine iliyonifanya kutokea kuipenda kompyuta hii ni uwezo wake wa betri na kwa hakika workstation ni muhimu kuwa na uwezo wa kukaa na chaji kama kwenye HP ZBook X2; kompyuta hii ina uwezo wa kukaa na chaji kwa saa kumi na ina wezo wa kujaa na chaji mpaka 50% kwa dakika 30 tu.

HP ZBook X2 inakuja ikiwa tayari imeshawekwa programu wezeshi (Adobe apps) kwa ajili ya kazi ya uhariri wa picha na video ikiwa pamoja na ofa ya kutumia kwa mwaka mmoja Creative Cloud bila malipo.

HP ZBook X2 tayari imeshazinduliwa na bei yake $1,749|Tsh. 3,933,501 ingawa itaanza kupatikana kuazia mwezi Desemba. Wachambuzi mbalimbali wanasema kompyuta/tabiti hii inalenga kuleta ushindani dhidi ya Microsoft Surface Pro na Surface Book. Je, wewe una mtazamo gani kuhusu hili?

Vyanzo: ZDNet, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Hili ndio toleo la Nokia 7
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|