Ifahamu Pikipiki Inayotumia Maji Badala ya Mafuta Nchini Brazili! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Ifahamu Pikipiki Inayotumia Maji Badala ya Mafuta Nchini Brazili!

0
Sambaza

Mbrazili mmoja ameshangaza wengi duniani baada ya kuunda pikipiki inayotumia maji kuendesha injini yake, pikipiki hiyo iliyopewa jina la T Power H2O imekuwa gumzo kubwa sio tu Brazili bali hata ulaya na America. Haijalishi kama maji ni machafu au maji ni masafi unacho hitaji ni kuyachuja na yatakua tayari kutumiwa.

where to purchase finasteride

CJ4oj3XWgAAlYZZ

source link T Power H2O, Picha ya Upande ikionesha tanki la maji na mfumo mzima wa mabomba kwaajiri ya kurumia maji kutengeneza nguvu ya kuendeshea.

http://resequipment.com/category/reviews/ Mfumo wa pikipiki hii unahusisha maji pamoja na betri ya gari, betri ya gari inasaidia kutenganisha haidrojeni kutoka katika maji. Baada ya kutenganishwa hydrogen hii hutumika kutengeneza nguvu inayoendesha pikipiki hiyo.

Pikipiki hiyo inaweza kwenda umbali wa kilometa MIA TANO kwa kutumia LITA MOJA TUU ya maji!

2AB7909000000578-0-image-a-22_1437494376616

Azevedo Akijaza maji katika tanki la pikipiki kabla ya kuanza kuiendesha.

Raia huyo wa brazil ambaye ni afisa jamii akielezea katika video hiyo amesema kuwa moja ya faida ya kutumia maji ni kwamba haktakuwa na uchafuzi wa mazingira maana shughuri hii hutoa mvuke na sio hewa ya kaboni monoksaidi.

2AB790A700000578-0-image-a-29_1437494423063

Azevedo hapa akiweka maji kutoka katika mto uliochafuliwa kuonesha kuwa hata maji yasiyo safi pia yanaweza kutumika.

Katika video hiyo  Azevedo anaonekana akinywa maji kuonesha kuwa kweli ni maji kisha kuijaza katika pikipiki, baadaye anaonekana akichota maji kutoka katika mto (uliochafuliwa) kisha anayajaza katika pikipiki na kuondoka. Hii siyo mara ya kwanza kwa kutengenezwa pikipiki ikatumia maji ila pengine hii inaweza kwenda mbali zaidi na kufikia hatua ya kutengenezqa kibiashara.

Upo hapo? Je unafikiri mataifa yenye kupata faida nyingi kutokana na biashara ya mafuta wanaweza kufurahisha na teknolojia kama hizi? Tupe maoni yako.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Leave A Reply