Ifahamu Smart Kicka kutoka Vodacom, Sifa Nzuri Kwa Bei Raisi

Ifahamu Smart Kicka kutoka Vodacom, Sifa Nzuri Kwa Bei Raisi

0
Sambaza

Vodacom_smart_kicka

Habari wadau! Tumewaeleza kwa undani kuhusu simu mbalimbali za gharama kama iPhone 6 lakini mwisho wa siku wengine hawapendi kununua simu za gharama sana, au kubwa sana. Pia hata wale wanaomiliki simu kubwa pia wanavutiwa na kumiliki simu ya pili kwa ajili namba nyingine na wanapendelea iwe ndogo. Ukiwa kwenye kundi hili, au pia kama sijagusia kundi lako naamini simu hii ya Smart Kicka kutoka Vodacom inaweza ikawa ni chaguo bora ukilinganisha sifa zake na bei ya kutupa inayouziwa.

buy line Seroquel Je hili ni dili la uhakika?

Hilo ndilo swahili muhimu ila kabla sijalijibu, tupitie vitu muhimu kuhusu simu hii.

Ndani ya boksi nimekuta chaja, simu na betri vikiwa vimetenganishwa, earphone pamoja 'earphones'

http://bonniesbocahomes.com/idx2/3715-Canterbury-Way-Boca-Raton-FL-33434-mls_RX-10235506 Ndani ya boksi nimekuta chaja, simu na betri vikiwa vimetenganishwa, earphone pamoja ‘earphones’

Loading

Video ya 1 – Muonekano wa boksi | Jiunge nasi pia kupitia Instagram @teknokona

View on Instagram

enter site Inakuja na Android 4.4.2, hili ni miongoni mwa toleo jipya kabisa la Android, na isikutishe ukafikiria jambo hili litaifanya simu hii kutokuwa kasi, yaani kuwa ‘slow.’ Simu hii inafanya kazi kwa kasi mzuri tuu na tunategemea hii inaweza ikawa kwa sababu imetumia toleo spesheli kutoka Google linalohakikisha hakuna vitu visivyokuwa vya msingi sana kama vile ilivyokuwa kwenye simu nyingi zilizotoka mwaka huu za kisasa kama Samsung Galaxy S5 na zingenezo. Nimeichunguza na kukuta inasehemu ya kutazama kama kuna sasisho (update) jipya.

Sehemu ya kufanya 'updates', kwa lugha yetu tunaita sasisho. Hii inapatikana kupitia eneo la 'Settings'

Sehemu ya kufanya ‘updates’, kwa lugha yetu tunaita sasisho. Hii inapatikana kupitia eneo la ‘Settings’

Ina uwezo wa Bluetooth na WiFI. Hii ikiwa na pamoja na kukuwezesha kutumia huduma ya ‘tethering’, ile ya kusambaza huduma ya intaneti kutoka kwenye simu ya kwako kwenda vifaa vingine.  Tena mtumiaji atafurahia zaidi huduma hii kwa kuwa simu hii inashika mfumo wa intaneti ya kasi wa 3G.

INAYOHUSIANA  Clickfarms: Wauza Likes, Shares, na Comments wakamatwa nchini Thailand

Kwenye kitengo cha kamera, ina kiwango cha kawaida (2 Megapixel) na hili ni jambo la kutegemea kwa simu ya chini ya Tsh 150,000/= ila bado ni kamera ambayo ni nzuri tu kwa matumizi ya kawaida kama kujipiga viselfi na kadhalika. Tumejaribu kupiga picha eneo lenye mwanga mdogo, kupitia chaguzi la ‘Night Mode’ yaani picha za usiku kwenye kamera na iliweza kutoa picha nzuri tuu. Haina ‘flash’, yaani taa ya mwanga unapopiga picha za usiku na eneo la giza. Hivyo kwa matumizi ya picha za kawaida inaridhisha sana tuu. ila fahamu jambo moja

Ndani ya boksi nimekuta chaja, simu na betri vikiwa vimetenganishwa, earphone pamoja 'earphones'

Muonekano wa Kioo-Nyumbani. Kama unavyoona kioo chake kina uwezo wa muonekano mzuri.

Inauzwa ikiwa tayari na apps maarufu kama Facebook ma Twitter

Inauzwa ikiwa tayari na apps maarufu kama Facebook ma Twitter

Kioo chake ni cha inchi 3.5, ambacho si kidogo sana kiasi cha kufanya utumiaji uwe wa shida. Maneno yanasomeka na kama unaona ni madogo bado unaweza kuongeza kupitia ‘settings’. Ni simu inayobebeka kwa uraisi na haisumbui kutumika mkononi, kwa ukubwa wa kipimo cha urefu wa mm 112 x upana mm 62 x na unene wa mm 12. Mguso (Touch) wa kioo chake unaridhisha na si wa kuzingua ukilinganishwa na ule unaokutana nao kwenye simu za bei raisi nyingi zilizopo sokoni.

INAYOHUSIANA  Snapchat waonja shubiri ya kupata hasara

Inakuja na apps mbalimbali kama Facebook, Twitter, Chrome, Gmail na nyinginezo nyingi. Utakuwa na uhuru wa kuongeza zaidi kupitia diski-uhifadhi ya simu hiyo yenye uwezo wa GB 4  na hii ni pamoja na kupewa nafasi ya kuongeza uwezo huo kupitia kadi ndogo (SD Card/Memory Card).

Ukifungua boksi linalokuja na simu hii unapata chaja, kitabu cha maelekezo zaidi (ila kwenye lugha ya Malkia Elizabeti) pamoja na ‘earphone’ zenye kiwango cha kurizisha. Kupitia utafiti wangu imetengenezwa na kampuni ya Arcatel kwa ajili ya Vodafone/Vodacom.

Simu hii inaweza kukuasaidia katika matumizi mbalimbali ya kila siku, na kutokana na kuja na Android 4.4.2 Kit Kat basi utaweza kutumia apps nyingi za kisasa. Magemu madogo mengi utaweza kuyatumia bila tatizo, tumejaribu kutumia intaneti na inafungua vizuri bila kuathiri muonekano.

Mtandao wa TeknoKona ulifunguka kwa uzuri sana kupitia Chrome. Kupitia ubora wa Android Kit Kat suala la intaneti tegemea kiwango kizuri sana.

Mtandao wa TeknoKona ulifunguka kwa uzuri sana kupitia Chrome. Kupitia ubora wa Android Kit Kat suala la intaneti tegemea kiwango kizuri sana.

Kwa sifa zote hizi tulizoangalia naweza kumalizia kwa kusema kwa bei husika, pamoja na kujumlisha 3GB za bure na dakika 1,200 hili ni dili la Uhakika. Kupitia ukurasa wao wa Facebook Vodacom wanasema simu hii unaweza ipata kwenye maduka yao. Pia kumbuka kuungana nasi kupitia Instagram – http://instagram.com/teknokona

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply