Infinix Zero 5 Pro: Simu janja mpya yenye kukaa na chaji siku mbili

0
Sambaza

Baada ya kuweka makala ya uchambuzi wa simu janja ya Infinix Note 4 Pro baadhi ya wasomaji wetu wa teknokona wameomba tuipitie simu nyingine kutoka kampuni ya Infinix inayofahamika kama Infinix Zero 5.

Simu janja hii ya Infinix Zero 5 ndio simu mpya na ya mwisho kutolewa na Infinix  baada ya Infinix Note 4 iliyozinduliwa mwezi Agosti mwaka 2017. Bila ya hiyana leo tunawaletea uchambuzi mfupi kuhusu simu janja hiyo.

Infinix Zero 5 ni simu janja mpya iliyozinduliwa mwezi Novemba mwaka 2017. Simu hiyo imekuja na ukubwa wa kioo cha nchi 5.98 chenye teknolojia ya IPS LCD (1920 x 1080 pixels).

>Kama ilivyo kwa Infinix Note 4, nayo Infinix Zero 5 ni simu kubwa, yenye uzito mwepesi iliyokuja na rangi tano ambazo ni nyeusi, dhahabu, shaba, nyekundu na kahawia. Bodi ya simu hii imetengenezwa kwa madini ya Aluminiam

SOMA PIA:  'ScreenShot' Bila Kutumia Kibonyezo Cha Kuzima Simu! #Android

>Fahamu simu janja hii ina matoleo mawili la Infinix zero 5 na Infinix Zero 5 Plus. Tofauti zake ni kwamba toleo la Plus litakuwa na ongezeko la diski hifadhi ya ukubwa wa 128GB. Tofauti nyingine ni katika bei ambapo Infinix Zero 5 itauzwa kwa dola 399 na Infinix zero 5 Pro itauzwa kwa dola 444.

>Prosesa yake ni ya 2.6GHz octa-core MediaTek Helio P25. Kwa upande wa ndani yaani diski uhifadhi (internal storage) ukubwa wake ni 64GB pamoja na RAM ya 6GB. Pia unaweza kuweka memori ya nje yenye ukubwa mpaka 128GB.

SOMA PIA:  Samsung kwa mwaka 2018: Kuuza mamilioni ya simu, Galaxy S9 ipo njiani

>Kwa upande wa wapenzi wa Kamera Infinix Zero 5 haijambo pia. Kamera ya nyuma zipo mbili moja ya 12-megapixel na nyingine ya 13-megapixel. Kamera ya mbele (Selfie) ina 16-megapixel. Kwa watu wa mapicha picha hapo kazi kwenu tu.

Kwa upande wa mfumo endeshi ni toleo la Android 7.0 Nougat ndio litakaloendesha simu hii, pamoja na Betri yenye ujazo mkubwa wa 4350mAh.

Kwenye suala la ujazo wa Betri hawa jamaa ni kama wamekomesha, ni ujazo mzuri ambao utamfanya mtumiaji wake kutokuwa na wasiwasi wa kuishiwa chaji kwa muda wa siku mbili mfululizo kwa matumizi bila ya kuchajiwa.

>Kwa wale ambao wana laini zaidi ya moja kwenye Infinix Zero 5 wameangaliwa kwa kuwekewa sehemu mbili za kuweka laini bila ya shida yoyote. Laini ambazo zinakubalia ni za Micro-SIM yaani laini ndogo za saizi ya kati. Ndio saizi inayotumika kwenye simu nyingi za Android.

SOMA PIA:  Simu janja ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya utengenezaji magemu

>Vitu vingine utakavyopata kwenye Infinix Zero 5 ni Fingerprint, Wi-Fi, GPS, Bluetooth, FM Radio, na inasapoti mfumo wa 3G na 4G.

Infinix ni watengenezaji wa simu walio na makao makuu yao huko nchini Uchina katika mji wa Pudong. Ilianza kutoa huduma tangu mwaka 2012 na maeneo makubwa ya biashara zake ni bara la Afrika na Asia. Pia, Infinix inadai kuwa matawi katika nchi zaidi  60 duniani kote.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com