Instagram wamechukua hatua ya kuongeza uthibitisho wakati wa kuingia katika akaunti ili kupunguza udukuzi, hivi karibuni kila unapoingia katika akaunti yako ya Instagram basi pamoja na kuandika anuani yako ya barua pepe yako na nywila utatakiwa kuandika namba ambayo itatumwa katika simu yako.
Hatua hii itafanya kwamba kuwa na anunai ya barua pepe na nywila isiwe kigezo cha kuweza kufungua ama kuingia katiak akaunti yako ya instagram bali utahitaji pia kumiliki simu iliyosajiliwa katika hiyo akaunti kwa wakati huo ili uwezae kupokea neno la siri la pili.
Watumiaji wengi wa mtandao wa instagram wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya udukuzi mara kwa mara na kupelekea kuwaingiza katika matatizo pengine na watu wao wa karibu au jamii kwa ujulma, hata hapa kwetu Afrika Mashariki tumekwisha ona watumiaji kadhaa wa mtandao huu wakiwa wahanga wa udukuzi mfano ni msanii Ben Pol aliwishawahi kufanyiwa udukuzi katika akaunti yake ya instagram.
Instagram kama ilivyo mitandao mingine inajaribu kufanya kila linalowezekana katika kuwalinda watumiaji wake dhidi ya wadukuzi mbalimbali, ikumbukwe kwamba Facebook tayari imekwisha anza kutumia huduma kama hii ambayo Instagram wanataka wailete.
Endelea kufuatilia mtandao wako wa Teknokona maana hapa tutakujulisha pindi hii huduma itakapo anza kutumika kwa watumiaji wote. Huduma itakapokuja itawasaidia saana watu hasa hapa kwetu Afrika mashariki ambapo mastaa wengi wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kwamba akaunti zao zimedukuliwa.
No Comment! Be the first one.