Kwa nini usafishe cache na data za android yako? #Maujanja

0
Sambaza

Kuongeza kasi ya simu na kupunguza ujazo wa kitumi cha mkononi ni mambo yanayofanyika mara nyingi hasa kwa wale wenye vitumi vya hali ya kawaida. Wachache hata hivyo huenda hawajui ujanja huu.

Je unafahamu kuhusu cache na data za android? Fahamu kwa nini kufuta mara moja moja kuna weza saidia simu yako kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Leo fahamu;

Kufuta Cache.

App nyingi hutumia intaneti huwa na kawaida ya kuhifadhi baadhi ya taarifa ili kuongeza kasi ya huduma iwapo data hizo zitahitajika tena. Kipengele hiki ndiyo kinachoitwa “cache”. Muda mwingi ukipita, taarifa hizo za kwenye simu zinapishana na zile za huduma husika na hatimaye huleta mkanganyiko unaopunguza kasi ya simu kupata huduma.
Hapa ndipo hitaji la kufuta cache linapokuja.

SOMA PIA:  Samsung yazindua Samsung Galaxy J7 Prime 2 kitofauti na ilivyozoeleka

Ingia kwenye settings>app settings>wipe cache.

Kufuta Data.

App nyingine, hasa za muziki na picha huenda mbele zaidi na kuhifadhi taarifa muhimu za mtumiaji, picha, video na muziki. Hii inakuwezesha kufurahia huduma zake iwapo intaneti itakata au haipo.

Kwenye app kama hizi unaweza kukuta kipengele kinachokuwezesha kuweka kikomo cha uhifadhi. Hata hivyo nafasi itapungua kwenye simu yako unapotumia app hizi muda mrefu na utahitaji kufuta data hizi ili kuongeza nafasi ya vitu vingine kufanyika kwenye android yako, kama kusasisha app.

SOMA PIA:  BoomPlay Music Yashinda Tunzo Ya App Bora Afrika! #AppsAfrica

Ili kufuta data hizi, ingia kwenye settings>app settings>chagua app>”wipe data”. Tambua kwamba utakapofuta data hapa, utalazimika kujiidhinisha (“sign in”) tena kwenye app husika.

cache na data za android

Hatua za kufuata

cache na data za android

Ingawa vipengele hivi ni huru na vya wazi kabisa kwenye androidi kuongeza kasi ya simu yako na kuokoa uhifadhi, zipo app ambazo zinakupa urahisi wa kutumia ujanja huu automatiki – yani bila wewe kuwa na haja ya kutumia muda mwingi kubonyezabonyeza simu yako. App hii ni kama CleanMaster ambayo tumewahi kuielezea -> Ifahamu app ya Clean Master

SOMA PIA:  Twitter kuongeza idadi ya maneno ya kuandika ujumbe

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com