Jinsi ya kusambaza kitu chenye ujazo mkubwa kwenye WhatsApp #Maujanja

0
Sambaza

Kutuma vitu kwa njia ya WhatsApp ni jambo lililozoeleka hivi sasa na hivyo watu wanaweza kutuma/kupokea kitu (nyimbo, picha, nyaraka, n.k) kwa njia ya WhatsApp bila tatizo lolote lakini kulingana na ukubwa wa kitu chenyewe.

Uwezo wa kutuma kitu ambacho kinazidi ukubwa wa MB 16 imekuwa ni changamoto kwa wale wote ambao walikuwa wanataka kumtumia mtu kitu chenye ukubwa unaozidi MB 16 hivyo basi mpango huo kushindikama kabisa. Lakini baada ya kuulizwa na moja ya wafuatiliaji wa TeknoKona kama inawezekana kutuma kitu ambacho kina ukubwa kuzidi na kile kiwango cha mwisho kilichowekwa na WhatsApp jibu ni ndio, inawezekana.

SOMA PIA:  Nokia 3310 (2017) ina Tatizo litakaloifanya kutonunuliwa kwa baadhi ya Nchi #Uchambuzi

Mbinu ya kutumia ili kuweza kutuma kitu chenye ukubwa unaozidi MB 16 kwenye WhatsApp.

Ukisema utumie mbinu ya kupunguza ukubwa (compress) utakuwa umeondoa vimelea fulani kwenye faili husika na hivyo kufanya kupoteza ubora ilikuwa nao kwamba ya kupunguzwa ukubwa hivyo, hatushauri utumie njia hii.

Njia ambayo ni nzuri na rahisi na ambayo haitaweza kufanya video husika kupoteza ubora wake ni kwa kutumia link ya video husika ambayo utaisambaza kutokea kwenye Dropbox na kisha kuituma kwa mtu ambaye unataka kusambazia video hiyo:

  1. Pakua app ya DropBox kutoka kwenye soko la Apple au Google. Pia, unaweza kupakua app ya Dropbox kwa kubofya>>Drobox-Android|Dropboox-iOS.
  2. Fungua app ya Dropbox na kisha bonyeza menyu ya kwenda chini halafu chagua “Share>>Copy link”.
  3. Chagua watu unaotaka kuwatumia hiyo video kwa kuwasambazia ille link ya ambayo umeinakili kutoka kwenye Dropboox.

Kwa yeyote yule ambaye utakuwa umemsambazia ile link akifungua tu ataweza kupakuwa hiyo nyaraka uliyomtumia kwenye simu yake bila kujali ukubwa wa kitu husika.

Maelezo ya hapo juu ni mojawapo ya njia zitakazokuwezwsha kutuma kitu chenye ujazo mkubwa ila kitu ambacho wengi hawakifahamu ni kwamba kwenye app-Telegram unaweza kutuma kitu chenye ujazo mkubwa (hata zaidi ya GB 2 🙄 🙄 ).

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com