Jinsi Ya Kushusha (Kudownload) Video Kutoka Facebook Moja Kwa Moja!

0
Sambaza

Tangia mtandao wa kijamii wa Facebook ulipoweka huduma/kipengele chake cha kuwawezesha watumiaji wake waweze kupakia na kuangalia video za aina mbalimbali kutoka katika mtadao huo  imekua ni safi sana. Watu sasa hivi wakiwa katika mtadao huu hawategemei ujumbe na picha tuu.

Kumbuka unaweza kuona video katika mtandao huo wa Facebook na ukatokea kuipenda sana, sasa kuna njia ya kuipata video hiyo ukiwa katika kivinjari chako bila hata ya kuwa na App nyingine ya kufanya zoezi hili (kushusha)

SOMA PIA:  Magwiji ya mitandao ya kijamii yaungana dhidi ya meseji za kigaidi

Kwa kufuata njia zifuatazo utaweza kushusha video kutoka katika mtandao wa kijamii wa Facebook na kuzihifadhi katika kompyuta yako bila ya kuwa na App nyingine mbadala.

  • Fungua mtandao wa facebook katika kivinjari (Google Chrome, Internet Explorer ndivyo tunavyopendekeza) na nenda mpka katika video unayoipendelea kuishusha
  • Bofya katika video hiyo kwa lengo la kuifungua kwa ukubwa (full screen)
  • Sasa katika sehemu ya kuandika tovuti inabidi ufanye mabadiliko kidogo kwa mfano kutoka https://www.facebook.com/video/xyz na kubadilisha kuwa https://m.facebook.com/video/xyz cha msingi hapa ni kwamba utaondoa www za mwanzo katika tovuti na utaweka herufi m (mwanzoni) na utabofya Enter.
SOMA PIA:  Kwa nini uchague au usichague simu za iPhone (iOS) badala ya Android?

Angalia Picha Kwa Kuelewa Zaidi

Mfumo wa simu wa Facebook ukiwa na hiyo video utatokea na kisha unaweza kubofya katika video hiyo ili ianze kucheza

Video ikishaanza kucheza unaweza uka ‘right click’ na kusha ukachagua Save video as…  katika machaguo ambayo yatajitokeza.

Katika ukurasa(window) mpya ambayo itatokea unaweza chagua sehemu ya kuhifadhia  video hiyo na unaweza hata kubadilisha jina la video hiyo (hapo utakuwa umeihifadhi video hiyo)

Video hiyo kutoka Facebook itaanza kujishusha na kujihifadhi katika kompyuta yako.

SOMA PIA:  BlackBerry yapata faida: Mapato ya biashara zake yazidi kukua

Ni matumaini yetu kuwa umeweza shusha video kutoka Facebook kwa urahisi kabisa. Kama kuna tatizo lolote lililojitokeza tuangikie sehemu ya comment na kisha tutaenda sawa na wewe. Tembelea mtandao wako pendwa kila siku.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com