Kijana Amtongoza Binti kwa iPhone 6 – MIA kasoro Moja!

0
Sambaza

iphone 6 chinaHaya sasa majanga! Wanasema upendo hauwezi kununuliwa kwa pesa, lakini hakika pesa inaweza kununua iPhone 6 tisini na tisa.. 🙂 Kijana mmoja huko China amekataliwa na binti mchana kweupe pale alipoandaa tukio la kumtongoza binti huyo kwa mbwembwe za kumnunulia iPhone 6 tisini na tisa!

Ilikuwaje?

Novemba 11 kwa utamaduni wa huko China ni siku ambayo wale walio peke yao a.k.a ‘singles’ wanafanya wawezavyo kuweza kuwapata wale wawapendao basi kijana huyo ambaye ni mprogramia wa kompyuta alijikita mfukoni na kutumia takribani milioni 14 za kitanzania kununua iPhone 6 99. Alizitumia iPhone hizo kutengeneza alama ya kopa (Love) <3 na alimualika binti huyo ndani ya kopa hilo na kumueleza yaliyomoyoni mwake akiwa amebeba maua mazuri mbele ya marafiki kibao….

SOMA PIA:  Teknolojia ya Face ID kwenye iPhone X yaendelea kukosolewa

Binti akasema hapana! Haiwezekani!

iphone 6 - china

Kijana akijitutufua! iPhone 6 99 zikiwa zimetengeneza kopa nzuriiii!

Pesa alizotumia ambazo ni takribani 500,000 yuan za huko nchini Uchina inakadiriwa kuwa ni karibia mshahara wa miaka miwili! Picha za kukatiliwa kwake na tukio ile zimeenea nchini humo baada ya tukio hilo…. 🙁

Kijana atalalia iPhone zake leo kwa majonzi kwelikweli 🙂

Kufahamu kuhusu simu za iPhone 6 BOFYA HAPA

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com