Mambo 6 Yasiyo ya Kweli kuhusu Kuchaji Simu - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mambo 6 Yasiyo ya Kweli kuhusu Kuchaji Simu

3
Sambaza

Kuna mengi sana unaweza ukawa ushasikia sana kuhusu njia nzuri za kuchaji simu yako. Pia utakuwa umeshasikia kuhusu ambayo hutakiwi kufanya ukiwa unachaji simu.

Je, yana ukweli wowote?

http://acousticbox.com/Banjo Anatomy and Assembly/parts7.htm

Leo tutakuelezea kwa uchache na kwa ukweli mambo muhimu kuhusu kuchaji kwa simu na usalama wa betri za simu wakati tukiwa tunazichaji.

Android kuchaji simu betri

1. Kutumia chaja ambazo si za makampuni ya simu zinaua simu

Hapana, hakuna ukweli kabisa katika hili ila ukweli ni kwamba usitumie chaja za ubora mbovu. Chaja feki si chaja zote ambazo hazitengenezwi na kampuni husika ya simu bali ni chaja ambazo zipo chini ya kiwango. Na hizi utazigundua kupitia bei zake, usikubali kumiliki simu ya gharama halafu ukawa mbahili katika kununua chaja za uhakika kisa bei zake.

Cha kufanya soma kuhusu kiwango na ubora wa chaja inayofaa kwenye simu yako kabla ya kununua chaja isiyokuja na simu yako.

INAYOHUSIANA  Ulinzi wa akaunti yako ya WhatsApp ni muhimu

2. Usitumie simu yako wakati unaichaji

Si kweli, ni kweli zamani sana, kwa sasa teknolojia inayotumika kwenye chaja na simu ni salama kabisa.  Cha kuhakikisha ni kwamba unatumia chaja zilizo na kiwango/ubora wa uhakika (original/quality). Kumbuka hapa haimaanishi ni kwamba lazima iwe ni yenye lebo/nembo ya kampuni husika bali hili ni suala la kuwa ni chaja yenye ubora wa uhakika.

3. Usizime simu yako kamwe!

Si kweli! Unashauliwa kuzima simu yake angalau ata mara moja kwa wiki kwa angalau lisaa. Simu kama vifaa vingine vyote vya umeme ni muhimu kupata muda wa kupumzishwa. Na jambo hili ndio linaboresha zaidi uhai wa simu yako.

4. Kuchaji simu usiku kucha kutaiua/haribu

Usisikilize hii…si kweli! labda kama unatumia simu iliyotengenezwa miaka ya 1980 :-). Teknolojia imekua sana, fahamu ya kwamba simu zote za siku hizi zitaacha kutumia umeme pale simu yako itakapochaji hadi asilimia 100! Itaacha kuchaji! Hakuna madhara! Ila hii haimaanisha ndio uiache kwa zaidi ya masaa 15! 🙂 na pia kuhakikisha unaichaji sehemu inayopata hewa 🙂

INAYOHUSIANA  Ondoa vitu kwenye Thumbnails kuongeza nafasi

5. Subiri hadi chaji iwe chini kabisa au imeisha ndio uchaji

Hili sio kweli! Ukweli ni kwamba kuchaji mara kwa mara ndio kunasaidia zaidi kuongeza maisha ya betri yako. Kumbuka kuchaji mara kwa mara si kila baada ya dakika 5, bali ni kwamba usisubiri chaji iwe chini ndio uchaji, na si lazima ukiweka kwenye chaji usiitoe hadi imejaa.

6. Kuna aina kuu mbili za mabetri yanatumika kwa sasa

Kuna mabetri yanayotumia teknolojia ya Lithium-Ion (Li-ion) na Lithium-Ion-Polymer (Li-ion polymer/Lithium Polymer). Kuna teknolojia nyingi zilizokuwepo zamani ila kwa sasa hizi ndio zinazotumika zaidi. Na zinatumika kutokana na ubora wake. Lithium-Ion (Li-ion) zinatumika zaidi katika simu nyingi zaidi wakati mabetri ya Lithium-Ion-Polymer yanatumika zaidi katika laptop na baadhi ya simu pia. Lithium-Ion-Polymer ndio teknolojia bora zaidi na salama zaid, lithium-Ion ni salama pia kwa kiwango kikubwa sana ila lithium-ion-polymer ni zenye ubora zaidi na hii inaweza kuwa ni sababu kubwa zinatumika kwenye laptop nyingi tayari. get link Teknolojia hizi zimefanya ulipukaji ovyo wa mabetri ya simu kuwa mgumu sana kuliko unavyofikiri. 

INAYOHUSIANA  Downloading vs Streaming : Fahamu Tofauti Kuu, Kipi bora zaidi?

Je ulikuwa unaamini nini kabla? Kumbuka kusambaza makala hii kwa wengine na pia unaweza ungana nasi kupitia  cheapest way to buy finasteride akaunti zetu za Twitter, Facebook na Instagram 

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

3 Comments

  1. Pingback: Madhara ya kulala na Simu yako ikiwa Imewashwa - TeknoKona

  2. Pingback: Kubadilisha betri la simu, Ukiona haya ujue muda umefika

  3. Pingback: Mambo 5 Yaliyobadilishwa na Teknolojia - Fahamu kama unavyoelewa ni sahii au si sahihi! - TeknoKona

Leave A Reply