Matatizo Ya iOS Yanayosumbua Zaidi (na Utatuzi wake)

0
Sambaza

Je unatumia iPhone ama iPad? ama unampango  wa kumiliki vifaa hivi siku za karibuni? Basi haya ni mambo ya muhimu kujua wakati unatumia vifaa hivyo. Yapo mambo mengi ambayo yanatukuta katika vifaa tunavyo tumia, hapa tutajadili matatizo yanayozikumba simu na tableti za Apple (ambazo zinatumia mfumo wa uendeshaji wa iOS).

Kuisha Chaji Katika Muda Mfupi.

Kama ilivyo kwa simu janja nyingi chaji pia ni changamoto katika vifaa vinavyotumia mfumo wa uendeshaji wa iOS, yapo mambo matatu ambayo unaweza kufanya ili kuilinda chaji ya iPhone ama iPad yako.

Moja; hakikisha unazima “background app refresh”, Background apps hupakia na kupakua data katika mtandao pia huendelea na shughuri nyingine hatakama hazijafunguliwa hivyo husababisha matumizi yasiyokuwa ya lazima ya chaji ya betri. Kuzima nenda katika settings>general>Background app Refresh na kisha zima hii huduma ama unaweza kuchagua kuzima zile huduma ambazo sio za muhimu zaidi.

SOMA PIA:  Ulinzi madhubuti wa kudhibiti barua pepe kudukuliwa (mtu mwingine kuitumia)

811837749_12866_15741025053924858153 (1)

Pili; zima baadhi ya huduma za maeneo(location services ) ambazo sio za muhimu kwako, baadhi ya huduma hizi zimewekwa ili kukufanya uifurahie simu/tableti yako lakini ukweli ni kwamba zinatumia chaji kwa kiwango cha juu isivyo kawaida. nenda settings>Privacy>location Services> System Services hapo zima Frequent Locations, Popular Near Me na  Location-based iADS

810618964_93362_16694116605260133665

Tatu; Angalia apps/vitumizi vyote ukitafuta vinavyotumia zaidi chaji ya betri yako na uangalie namna yakupunguza matumizi yake.

iPhone ama iPad kupoteza kasi katika kufanya mambo.

Katika hali ya kawaida kifaa inafaa kiwe na mwendo, hasa katika kufanya mambo mbali mbali hakitakiwi kiwe kina nasa nasa na kufanya mambo taratibu. Daima simu ama tablet yako hupunguza mwendo wa kufanya shughuri zake kadiri inavyojaa picha miziki ama apps, basi ni muhimu kuhakikisha hakuna kitu chochote ambacho hukihitaji katika simu/tablet yako. Nenda settings > General > Usage > Manage Storage na hapautaweza kufuta kila kitu usicho kitaka iwe ni kitumizi wimbo ama picha.

SOMA PIA:  Mambo 10 ya ujanja ujanja unayoweza kufanya kwenye iPhone 6/iPhone 6+

811833219_54467_9479106666915651573

Pia unaweza kupunguza manjonjo ya namna vitumizi (application) vinafunguka, iPhone na iPad huja na mpangilio ambao hufungua vitumizi katika namna ya kipekee yenye kufurahisha kwa bahati mbaya ni kwamba hii ni namna nyingine ya matumizi mabaya ya chaji ya betri. Kuzima hii nenda settings > General > Accessibility  hapa washa Reduce Motion 

811823963_58705_2426001846346032726

Matatizo ya kuunganisha na Mitandao.

Huwa inatokea mara nyingi unakifurushi cha kutosha cha intaneti lakini hauwezi kufungua mtandao, ama umeunganisha katika wi-fi yako lakini bado hauwezi kufungua mtandao. wakati mwingine hili sio kosa la mtandao unaotumia (ingawa ukweli ni kwamba asilimia 90 ya watu hudhani mtandao wao ndio wenyeshida) hivyo unashauliwa kuzima data ama Wi-Fi kisha kuwasha Airplane mode kwa muda wa dakika moja na baada ya hapo rudia kuwasha data yako au Wi-Fi iwapo tatizo litaendelea basi nenda hatua ya pili ambayo ni ku-reset mpangilio wa mtandao hii utaipata hapa Settings > General > Reset > Reset Network Settings

Skrini Ku-stuck ama Kuganda.

SOMA PIA:  Namna ya kuweka Play Store katika simu zenye mfumo wa kichina

Iwapo simu yako inaganda katika ukurasa fulani wa simu na haikubali kila unachobonyeza basi njia nyepesi na ya moja kwa moja kutatua tatizo hilo ni pamoja na kuizima na kuiwasha simu yako tena. Na pia hakikisha simu yako inaenda na wakati na matoleo yanayotolewa na apple kila wakati.

SOMA PIA – Mambo Ambayo Steve Jobs alisema Apple hawatayafanya na sasa wanayafanya!

Natumai hii itakusaidia kuifurahia simu yako ya iPhone ama iPad yako.Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com