Mauzo ya bidhaa za Apple zenye rangi nyekundu - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mauzo ya bidhaa za Apple zenye rangi nyekundu

0
Sambaza

Vitu mbalimbali zenye rangi nyekundu kutoka kampuni maarufu na tajiri katika biashara ya vifaa vya teknolojia. Apple imeonekana kupata mamilioni ya dola za kimarekani yaliyotokana na kuuza bidhaa zake zenye rangi upendo 😀 😀 .

click

Katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Apple iliweza kukusanya jumla ya $160 milioni yaliyotokana kuuza vitu kama iPhone, saa, n.k ambazo ni za rangi nyekundu na pesa hizo zote walizitoa kama mchango wao kwa Global Fund-shirika la kimataifa linalojishughulisha na kupambana na kuzuia maambukizi ya VVU.

buy online Proscalpin 1 mg Mauzo hayo jumla ya $30 milioni yalipatikana katika kipindi cha mwaka mmoja peke yake ambapo pesa hizo zilitokana na kuuzwa kwa bidhaa mbalimbali za Apple zenye rangi nyekundu. Kwa kiwango hicho cha fedha, Apple imeweka rekodi ya kupata kiwango cha juu ambazo fedha hizo zote zilitolewa kwa Global Fund ndani ya mwaka mmoja.

Kiwango cha $30 milioni ni sawa na siku 144 milioni ya dawa za kufumbaza makali ya VVU.

Kampeni ya bidhaa za rangi nyekundu.

Kampeni hii ambayo kwa Kiingereza inafahamika kama “The (RED) initiative” ilianzishwa mwaka 2006 na Bw. Bobby Shriver pamoja na U2’s Bono ikiwa na lengo la kushirikisha sekta binafsi na makampuni kama Apple, Nike kutengeneza bidhaa za rangi nyekundu na source site kiasi cha mapato yatakayotokana na mauzo ya bidhaa hizo yatatolewa kwa shirika la Global Fund.

Bidhaa mbalimbali za Apple za rangi nyekundu: Apple imechangia zaidi ya $160 milioni kwa Global Fund katika kipindi cha miaka 11.

Tangu kuanzishwa kwa kampeni ya bidhaa za rangi nyekundu shirika la Global Fund limekusanya jumla ya $500 milioni kwa ajili ya mapambano dhidi ya VVU.

Katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani kwa mwaka 2017 maduka ya Apple zaidi ya mia nne yaliwekwa nembo ya Apple ya rangi nyekundu. Apple imechangia dola moja ya kimarekani kwa kila bidhaa iliyolipiwa kwa njia ya Apple Pay, mtandaoni au kupitia kwenye app yao.

Ni jambo la kupendeza kuona makampuni makubwa yanatoa mchango wao katika mapambano dhidi ya VVU. Vilevile wananchi walipata nafasi ya kujionea jinsi bidhaa za Apple zenye nyekundu zinavyotengenezwa kwenye maduka ya Apple.

Vyanzo: Gadgets 360, Apple

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Vidokezo vya kwenye Samsung Galaxy Note 9
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.