Miundombinu ya TEHAMA na intaneti nchini Tanzania #Uchambuzi #Ripoti - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Miundombinu ya TEHAMA na intaneti nchini Tanzania #Uchambuzi #Ripoti

1
Sambaza

Matumizi ya TEHAMA nchini Tanzania yameonekana kukua na kutumia katika maeneo mengi tofauti na ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita. Baada ya kuhudhuria kongamano lililowakutanisha wataalamu na wadau wa TEHAMA mwezi uliopita tumejifunza mengi ya kujivunia.

Utakubaliana nasi kuwa mwenendo wa sasa kwenye TEHAMA nchini Tanzania ni tofauti sana na hapo awali na hii inatokana na serikali ya nchini Tanzania kuamua kwa juhudi kabisa kuwekeza upande wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo mpaka hivi sasa matumizi ya TEHAMA yameonekana kuwa na manufaa sana kwa serikali na wananchi kwa ujumla.

Kongamano la teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) kufanyika Oktoba 26 na 27 jijini Dar Es Salaam

Kwa takwimu za hivi karibuni tulizozipata kutokana na kuhudhuria kongamano inaonyesha kuwa Tanzania ipo katika nafasi ya kujivunia sana kwenye upande wa TEHAMA na tunapoelekea ndio pazuri kabisa kutokana na serikali ya Tanzania kuendelea kuweka nguvu nyingi sana kwenye TEHAMA.

Tanzania ilipo hivi sasa na inapoelekea kwenye upande wa TEHAMA.

Ilipo Tanzania

Kuwa na miundombinu mizuri na ya kisasa ndio sababu mojawapo ya kuifanya Tanzania kuwa katika nafasi nzuri katika TEHAMA ikiwa na takribani yanya za kisasa zaidi zinazotumia kwenye mawasiliano (optical fibres) ambazo zimesambaa urefu wa buy generic amoxil Km 27,000; Km 18 elfu kati ya 27 elfu ya optical fibres inamilikiwa na mtandao wa simu wa Halotel.

Kama ulikuwa ufahamu basi tambua ya kuwa hivi sasa Tanzania minara ya mawasiliano ipo nchi nzima kwa 94% huku makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano yakiwa saba kwa ujumla wake. follow url Kwenye masuala ya matumizi ya intaneti, imefahamika kuwa kuna watumiaji wa intaneti zaidi ya asilimia 40.

miundombinu ya tehama

Habari picha: Takwimu za mtandao wa simu ha Halotel. Mtandao wa simu ambao hauna hata miaka mitano tangu uanze kufanya kazi nchini Tanzania lakini umeweza kuenea sehemu kubwa nchini humo.

Inapoelekea Tanzania

Yalizungumzwa mengi sana kwenye kongamano kuhusu wapi Tanzania inaelekea tunapozungumzia TEHAMA lakini kwa uchache inapoelekea Tanzania kwenye masuala ya TEHAMA ni kama ifuatavyo:-

INAYOHUSIANA  Ijue simu mpya ya Honor Play 7

where can i buy erythromycin gel Kwa serikali

  • Kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na mfumo madhubuti wa masuaka ya TEHAMA utakaojumuisha miundombinu ya mawasiliano, intaneti.
  • Kuhakikisha kuwa mitaala ya kuhusu sheria ya masuala ya TEHAMA infundishwa mashuleni kutoka ngazi ya chini ya elimu hadi elimu ya juu ili kuwajenga na kufahamu sheria mbalimbali za TEHAMA na kuweza kujiepusha na yale makosa mbalimbali ya kwenye mtandao na yanayoshahabiana na TEHAMA.
  • Kuhakikisha pato la taifa (GDP) linalotokana na linaongezeka kwa 0.3% kufikia mwaka 2021.

Kwa wanachi, mawasiliano na mazingira

  • Kuhakikisha kuwa 50% ya wananchi wanafahamu kuhusu TEHAMA kufikia mwaka 2021 ilikwemo kuhakikisha mpaka kufikia mwaka 2021 asilimia 90 ya makampuni yote Tanzania yanatumia “.tz” kwenye wavuti zao na TeknoKona tayari tumeitikia wito huo; unaweza pia kutupata kupitia teknolojia.co.tz au teknokona.co.tz.
  • Kuhakikisha watu wenye ulemavu wana uelewa mpana wa masuala ya kidigiti na sio kujiona wameachwa nyuma katika kuwafanya wapate kujua na kuelewa suala zima la TEHAMA.
  • Kuwa na miundombinu ambayo ni salama na kuwa ngumu kushambuliwa na virusi, wadukuzi na vitu vingine.
  • Kuwa na viwanda vidogo vidogo vya kuweza kufanya bidhaa zilizotumika kuweza kuweza kutumika tena (recycling).
  • Kuwa na uwezo wa hali ya juu sana (National broadband) kama taifa kufikia mwaka 2018.

    Mitandao ya simu nchni Tanzania na teknolojia ya vizazi vya mawasiliano.

Kwa siku mbili TeknoKona ilipata fursa ya kuhudhuria kongamano la kwanza kabisa la masuala ya TEHAMA na kuweza kukusanya taarifa mbalimbali ambazo tutazidi kuwafahamisha katika siku za usoni. Je, Tanzania ilipo hivi sasa kwenye TEHAMA inafanya vyema au bado tupo kule kule ilipotokea?

Chanzo: AIPC na ICTC

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|