Ongeza Kasi Ya Internet Ya Kompyuta Yako!

0
Sambaza

unlimited-high-speed-internet-8

Technolojia inakua kwa kiasi kikubwa hivi sasa, hata spidi ya internet. Kuna baadhi ya watu bado wanapata shida katika suala zima la internet kwamba ina spidi ndogo kulingana na matakwa yao. teknolojia ndio iliyotuletea internet sasa kwa nn teknolojia inaongezeka lakini spidi ya internet ni ndogo hasa kwa bara la afrika. Kuna njia mbili za kuweza kutatua hili na mtumiaji itambidi achague njia moja kati ya mbili. Hapa inabaidi uchague ile yenye urahisi kwako japokua zote ni rahisi

NJIA ZA KUONGEZA KASI YA INTERNET

Kwanza kabla ya kuendelea mbele hebu angalia uwezo wa speed ya kompyuta yako hapa ili kujua kama mwishoni baada ya kutumia njia hizi utapata majibu tofauti

SOMA PIA:  Google kuleta mabadiliko kwa watumiaji wa simu.

 

NJIA YA KWANZA

  • Andika “gpedit.msc” katika kibox cha “Search for program and files”  kwenye menyu ya windows na itatokea window nyingine ya Local Group Policy Editor

increase-internet-speed-window

  • Ndani ya window hiyo iliyotokea upande wa kushoto, tafuta  Administrative templates chini ya  Computer Configuration ibofye na utaona settings upande wa kulia

  • bofya mara mbili (double click) Network na tafuta QoS Packet Scheduler na kisha fungua

  • Orodha ya settings itatokea upande wa kulia. jaribu kufungua Limit reversible bandwidth window mpya itatokea lakini muda huu chagua disable katika machaguo yatakayotokea

  • Bofya Apply alafu Ok

increase-internet-speed-disable

Hapo haina haja ya kuangalia spidi ya internet kama imeongezeka nna imani unaweza tuu kuhisi mabadiliko kama imeongezeka. lakini pia unaweza ukaangalia mabadiliko katika ile website ya speed test niliyokupa hapo awali

SOMA PIA:  Uangalie Nini Unapofanya Maamuzi ya Kununua Laptop? - (2017)

SOMA PIA: Mbinu 10 Za Kutumia Internet Kwenye Kompyuta!

 

NJIA YA PIILI

  • Fungua command prompt katika compyuta yako au andika Cm katika menyu ya kompyuta yako  a kisha itafunguka. Kisha andika ipconfig/all

  • Ita orodhesha taarifa zote za internet ya compyuta yako. Sasa Angalia internet connection ambayo unataka kuongeza spidi  na utaweza kuona IP Address ya internet yako

  • Kopi IP Address hiyo. Fungua window ya RUN kwa kuandika RUN katika “Search for programs and files” katika menyu ya windows

  • RUN ikifunguka andika ping <ip address> -t mfano ping 123.45.678.999 –t

  • Bofya OK na utaona command prompt ambayo pinging yaIP Address ya internet yako imeanza. Funga Command Prompt ya mara ya kwanza na kisha acha command prompt mpya iendelee. Angalia Spidi ya internet yako itakua imeongezeka

SOMA PIA:  Jinsi gani unaweza kuigawanya diski uhifadhi #Maujanja

 

Njia zote zinafanya kazi vyema mpaka sasa. Teknokona inashauri kutumia njia ya kwanza kwa sababu inaleta majibu ya uhakika zaidi na ni rahisi kutumia kuliko hii ya pili. Hata hivyo unaweza jaribu njia zote mbili na kuangalii ipi inakusaidia zaidi katika suala zima la kuongeza spidi ya internet yako

Tuambie njia hizi umezipokea vipi? je Zimekusaidia?  pia tembeleza kurasa zetu za Twitter, Facebook na Instagram upate makala za kijanja

 

SIKU NJEMA!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com