KENYA: Mauzo Ya Simu Janja Yatatawala Simu Za Kawaida 2017! #Utafiti

0
Sambaza

Kutokana na tafiti zilizofanywa na kampuni kubwa kabisa katika maswala ya utafiti (uchunguzi) wa data mbali mbali na uchambuzi imegundulika kuwa simu janja zimeenea kwa kiwango kikubwa.

Kampuni ya Global Data ni kampuni ya 4,000 kwa ukubwa duniani na katika ripoti yake imesema kuwa mpaka kufikia mwisho wa mwaka 2017 ni kwamba wakenya takribani milioni 20.1 watakua wameshajiunga na matumizi ya simu janja.

likitokea hilo basi bila shaka hii inamaanisha kuwa matumizi ya simu janja ndio yatakuwa yanaongoza ukilinganisha na matumizi ya zile simu za kawaida.

SOMA PIA:  India yashika nafasi ya pili kwa soko la mauzo ya simu za Android Duniani

Ongezeko la matumizi  kwa mwaka huu ni asilimia 16 ukilinganisha na mwaka uliopita. Hii ukifuatilia vizuri utagundua kuwa hili limetokea kwa sababu kuna ongezeko la simu janja nyingi ambazo zinauzwa kwa bei ya chini kabisa.

Jinsi Ongezeko La Manunuzi Ya Simu Janja Linavyotabiriwa Kupanda

Takwimu Zikionyesha Ongezeko La Matumizi Ya Simu Janja

Pia Global data imeweka wazi kuwa mpaka kufikia mwaka 2022, takribani asilimia 80 ya waKenya wote watakuwa wanatumia simu hizo.

Hili ni jambo jema kwa wakenya kwani matumizi ya simu janja kwa kushirikiana na intaneti huwa yanasaidia mambo mengi sana hasa hasa katika upande wa kukuza uchumi.

SOMA PIA:  Simu za Samsung Galaxy kuanza kupata toleo la Android Oreo 2018

Chanzo: Global Data

Ningependa kusikia kutoka kwako, hili umelipokeaje? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Diama Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com