Samsung Wakuletea Diski ya TB 1 SSD Inayotosha Kiganjani

0
Sambaza

Kampuni ya Samsung yaja na diski yenye umbo dogo zaidi lakini yenye ujazo mkubwa zaidi wa data ukilinganisha na umbo lake. Na zaidi ya yote diski hizi zinakuja katika mfumo wa teknolojia ya SSD (Solid State Disk – kama ile ya kwenye flashi diski), hii ikiwa ni tofauti na diski za pembeni  nyingi zilizopo sasa zinazotumia teknolojia ya HDD.

Teknolojia ya SSD ni bora zaidi ya ile ya HDD, diski za mfumo wa SSD zinafanya kazi kwa kasi zaidi na pia haziaribiki kwa urahisi.diski-ssd-samsung-external

Wakitambulisha diski hizo kwenye maonesho ya kiteknolojia huko nchini marekani Samsung wamesema diski hizo zitaingia sokoni baadae mwaka huu na zitegemewe kufika sokoni mwisho wa mwezi huu na zitaanza kupatikana katika nchi za ulaya, marekani, na asia kabla ya kusambaa zaidi.diski-ssd-samsung

Utaweza kuhamisha mafaili kutoka kwenye kompyuta kwa spidi ya zaidi ya mara 100 zaidi kulinganisha na diski ze nje (External) za mfumo wa Hard Disk Drive (HDD). Hii inamaanisha utaweza kuhamisha faili la GB 3 kwa sekunde 8 tuu na faili la GB 10 kwa sekunde 27 tuu.

Diski hizi ambazo Samsung wamezipa jina la ‘Samsung Portable SSD’ na jina litakuwa linamaliziwa kulinganisha na ukubwa wa uhifadhi wa diski husika, na kwa kuanzia Samsung wanakuja na diski za GB 250, GB 500 pamoja na TB 1.

SOMA PIA:  Gerard Pique wa Barcelona ahudhuria uzinduzi wa mkutano wa MWC

samsung-ssd-DISKI

Bei inayotarajiwa;GB 250 – $180 (Tsh 312,000/=), GB 500 – $300 (Tsh 520,000), TB 1 – $600(Tsh 1,040,000/=). Wengi wanategemea bei hizi zitaendelea kushuka pale kampuni nyingi zaidi zikijikita katika teknolojia hii pia.

Soma Pia: Diski ya TB 8 Kutoka Seagate Yaingia Sokoni

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com