Simu janja ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya utengenezaji magemu - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Simu janja ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya utengenezaji magemu

0
Sambaza

Katika mchezo ambao umekuwa hauna rika (hasa ughaibuni) uchezaji wa magemu ni moja kati ya michezo hiyo na kampuni ambayo daima imekuwa ikitengeneza magemu, kwa mara ya kwanza imeamua kuja na simu janja.

Kulikuwepo funuunu na mwisho ikawa gumzo tangu mwezi Julai 2017 kwamba Razer (kampuni) inatarajia kuja na simu janja ya kwanza kutoka kwao na yeyote ambaye ni mpenzi na mfuatiliaji wa magemu lazima atakuwa anajua kuwa Razer kwa miaka mingi imekuwa ikitengeneza magemu yaliyotokea kupendwa sana na kujizolea umaaruufu sehemu nyingi duniani.

Fahamu sifa za simu janja ya kwanza kutoka Razar.

 Simu janja nyingi zilizotoka katika miaka ya karibuni karibu zote zinatofautiana sehemu ndogo sana hasa kwenye buy celebrex in the uk RAM, diski ujazo, ukubwa wa kioo na uwezo wa prosesa iliyopo kwenye simu husika.

buy femara online cheap Kioo/Prosesa. Kiujumla simu janja ya Razar hawajatofautiana sana na simu janja zingine ambazo tayari zipo sokoni. Kioo cha kwenye simu hiyo kina ukubwa wa inchi 5.7 (2,560 x 1,440 resolution) huku ikiwa na prosesa ya order Dilantin canada Qualcomm Snapdragon 835.

Kumbuka kuwa simu janja hii imetengenezwa na kampuni ambayo inajihusisha zaidi na masuala ya magemu hivyo kitu kama graphics chip ni muhimu kuwa yenye ubora wa aina yake, simu hii inatumia Qualcomm Adreno 540 (sawa na ya kwenye Samsung Galaxy S8).

Diski ujazo. Kwa hakika ujazo wa simu hii utasaidia sana kwa wale wapenzi wa kuwa na magemu yenye ujazo mkubwa kwenye simu zao, inakuja na diski ujazo wa GB 64.

Simu janja ambayo ni nzuri sana kwa kucheza gemu; imetengenezwa na Razer-kampuni inayojihusisha na utenenezaji magemu.

Kamera. Moja ya vitu ambavyo kampuni nyingi inazingatia na kujitahidi kuwa simu zao zinatokea kuteka soko la simu janja, kamera ni moja kati ya vipengele hivyo na kwenye simu janja ya Razar kamera yake ina MP 12 (kamera ya nyuma) na MP 8 (kamera ya selfie).

Programu endeshi. Simu hii inatumia programu endeshaji kutoka Android nainakuja na toleo la Android 7.1.1. Ingawa toleo la Android 7.1.1 si toleo la hivi sasa ila simu hiyo itakuwa na uwezo wa kupokea masasisho na kuwa na Android 8 (Oreo).

Simu janja kutoka Razer imejidhatiti hasa kwenye RAM, ina RAM GB 8 (kuepuka kukwamakwama unapokuwa unacheza gemu) ambayo ni RAM ya kiwango cha juu sana kulinganisha na simu janja nyingi zilizotoka hivi karibuni ambazo zenye kiwango cha juu kabisa ni GB 6.

Tanzama picha ifuatayo kujua sifa nyingizo za simu janja ya kwanza kutoka kampuni iliyojikita zaidi kwenye utengenezaji wa magemu:-

Sifa za simu janja ya kwanza kutoka Razer.

Hakuna mengi yaliyoweza kufahamika (bei, picha) kuhusu simu janja hii kutoka Razer kutokana na kwamba taarifa zilizopatikana ni baada ya taarifa hizo kuvuja lakini imeelezwa kuwa simu hiyo itazinduliwa Novemba 1.

TeknoKona itaendelea kufuatilia kwa karibu zaidi kuhusu simu hii kutoka Razer ambayo inaonekana kuwa gumzo hata kabla ya uzinduzi wake.

Vyanzo: The Verge, Techradar, Mashable

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Ukuaji wa teknolojia katika kamera za kwenye simu
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.