SPACE X Yashindwa Jaribio lake la Kutua Roketi katika Meli - TeknoKona Teknolojia Tanzania

SPACE X Yashindwa Jaribio lake la Kutua Roketi katika Meli

2
Sambaza

Kampuni ya Space X inayowekezwa mabilioni ya dola za kimarekani katika kutengeneza na kutumia teknolojia ya kurudisha roketi salama duniani baada ya kupeleka mizigo nje ya dunia yapata pigo baada ya mpango wao wa kurudisha salama roketi kubwa kushindikana.

Mwishoni mwaka jana kampuni ya kimarekani ya Space X ilifanikiwa kurusha roketi ndogo iliyobeba setelaiti 11 na baada ya kuziweka setelaiti hizo roketi hii ilirudi na kutua kwa kusimama ardhini.

Biashara ya kupeleka satelaiti angani nje kidogo ya dunia (orbit) ni biashara ya mabilioni ya pesa

Biashara ya kupeleka satelaiti angani nje kidogo ya dunia (orbit) ni biashara ya mabilioni ya pesa

Baada ya hilo jaribio kufanikiwa Space x walitaka kujaribu kutua roketi katika meli, lakini jaribio hilo halikufanikiwa baada ya roketi hiyo kuvunjika mguu mmoja wakati ikitua.

Hapo juu ni video inayoonesha kwa ufupi misheni hiyo ya kuirudisha roketi hiyo ya falcon 9 duniani katika chombo maalumu kinachoelea baharini

INAYOHUSIANA  Sababu 5 kwanini ndege inapata ajali

Space x walipata ushawishi mkubwa baada ya mafanikio ya jaribio lao la kutua roketi hiyo ya Falcon 9 nchikavu lililofanyika mwishon mwaka jana. Hata hivyo safari hii mambo hayakuwa mteremko kwani baada ya roketi hiyo iliyokuwa imebeba satelaiti ya mambo ya hali ya hewa kufanikiwa kuufikisha mzigo wake ilirudi na kufanya jaribio la kutua katika meli iliyokua baharini ilifanikiwa kuanza kutua ila ilivunja mguu mmoja na kuanguka kisha kulipuka.

go to link Kuna faida gani kurudisha roketi iliyotumika salama!?

Mmiliki wa kampuni hiyo ya Space x Elon Musk anasema kwamba kuweza kurudisha duniani roketi iliyotumika ikiwa salama kutapunguza saana gharama za uendeshaji za kampuni yake na hiii itashusha gharama za kurusha roketi.

Roketi ya Space X ilipokuwa inatua baada ya kupeleka satelaiti angani. Mguu wake mmoja ulivunjika na hivyo roketi hiyo kuanguka na kulipuka wakati inatua.

Roketi ya Space X ilipokuwa inatua baada ya kupeleka satelaiti angani. Mguu wake mmoja ulivunjika na hivyo roketi hiyo kuanguka na kulipuka wakati inatua.

Wataalamu wa mambo wanasema kwamba hii ikifanikiwa itakakuwa ni hatua madhubuti katika lengo la wanadamu kwenda kufanya makazi katika sayari ya Mars.

INAYOHUSIANA  Ijue ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner

Mmiliki wa kampuni hiyo ya Space x aliposti video ikionesha jinsi roketi hiyo ilivyoshindwa kutua baada ya moja ya miguu yake kushindwa kufunguka ipasavyo na hatimaye kupelekea kuanguka na kulipuka. Hata hivyo bosi huyo amekuwa na matumaini kwamba walau roketi hiyo ilikaribia kufikia hatua ya mwisho.

Japokuwa jaribio la kutuoa katika meli limeshindwa lakini waswahili wanasema kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi, tunaaamini Space x hawajakata tamaa na wataendelea kujaribu tena na tena hadi watakapoweza kurudisha roketi duniani na kutua katika mazingira yeyote yale yaani baharini ama nchikavu.

Lengo kubwa hapa ni kuweza kutua katika madhingira yeyote na ikiwezekana kuweza kutua katika sayari nyingine, pengine miaka ijayo tutaweza kusafiri na kwenda sayari nyingine kama vile tunaenda Mwanza na ndege.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

2 Comments

  1. Pingback: SPACE X yafanikiwa kutua Roketi katika Meli! #Teknolojia - TeknoKona

  2. Pingback: Space X yafanikiwa kutua roketi katika Meli tena. - TeknoKona

Leave A Reply