Tecno Camon i Sky: Simu janja nyingine sokoni - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Tecno Camon i Sky: Simu janja nyingine sokoni

1
Sambaza

Transsion Holdings ni moja ya kampuni zinazoongoza kutoa simu janja mara kwa mara; moja ya bidhaa ambazo zipo chini ya kampuni hiyo ni Tecno na kwa hakika zina wateja wengi sana barani Afrika.

Tecno wana sifa lukuki na yote hii inatokana bidhaa zao ambazo bei yake ni ya kustahimilika; simu rununu ya Tecno Camon i Sky imezinduliwa tayari kumfikia mteja. Kama kawaida ya bidhaa za Tecno kuangalia na wale wenye uwezo wa kawaida, simu hii sio ghali na uwezo wake ni wa kawaida ila ina mfumo wa usalama wa click kufungua simu kwa kutumia sura.

Sifa/Uchamubuzi wa Tecno Camon i Sky.

Aina ya prosesa na uwezo wake.

Prosesa nzuri ndio sifa mojawapo ya simu/bidhaa husika kuwavutia wengi. Kwenye Tecno Camon i Sky kuna quad-core MediaTek MT6739WA SoC yenye 1.28GHz. http://aokstudios.com/wp-login.php Haina prosesa kubwa lakini simu hii imelenga zaidi wale watu ambao hawana matumizi makubwa sana na simu zao mathalani kuweka app/programu zenye kuchukua ujazo mkubwa kwenye simu.

INAYOHUSIANA  Facebook katika ulimwengu wa mahaba

Ukubwa wa kioo/Mfumo endeshi.

Simu za mguso ni muhimu kuwa na kioo ambacho ni kipana kwa wastani ili yule anayeitumia basi asipate tabu wa kubonyeza eneo/herufi husika. Simu hii inayozungumziwa hapa ina kioo chenye ukubwa wa inchi 5.45 na uwiano wa kioo ni 18:9 na programu endeshaji iliyopo kwenye simu hii ni Android 8.1 Oreo.

Simu janja nyingine

Tecno Camon i Sky inapatikana katika rangi nyeusi na dhahabu ambayo haijakolea.

RAM/Diski uhifadhi.

Huwezi ukazungumzia undani wa simu/kompyuta halafu usiongelee diski uhifadhi na RAM ya kwenye kifaa husika. Sababu ikiwa ni RAM inawezesha kifaa kutochukua muda mrefu kufanikisha jambo fulani; follow simu/kompyuta ikiwa na RAM kubwa basi itakuwa haikwamikwami katika utendaji wake wa kazi. Tecno Camon i Sky ina RAM GB 2 na diski uhifadhi GB 16 (unaweza pia ukaweka memori kadi).

INAYOHUSIANA  JIHUDUMIE: Huduma mpya kubatilisha muamala

Kamera/Betri

 Katika miaka ya karibuni, ukiwa na simu janja halafu uwezo wake wa kamera ukawa ni wa chini mfano chini ya MP 5 au isiwe na kamera ya mbele kwa ajili ya kujipiga picha (selifie) basi simu hiyo inakuwa kwenye kundi la simu za hali ya chini. simu ya Tecno Camon i Sky ina MP 8 za kamera ya mbele na MP 13 kamera ya nyuma. Kamera ya mbele ina flash 2 kumfanya mtumiaji apige picha nzuri za selfie au wakati wa kufanya mawasiliano kwa njia ya picha jongefu. Kamera ya nyuma ina flash kama kawaida.

Unapozungumzia uhai wa simu kwa asilimia kubwa ni uwezo kifaa chenyewe kutunza chaji kwa muda mrefu na linapokuja suala la simu janja kuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu hapa makampuni mengi huwa wanashindwa kwenye kipengele cha betri. Tecno Camon i Sky ina betri lenye 3050mAh.

Mengineyo

Tecno Camon i Sky ina uzito wa gramu 137, wembamba wake ni 147.5x70x8.3mm. Pia ina 4G VoLTE, ViLTE, GPS, Wi-Fi, Bluetooth, 3.5mm headphone jack, ulinzi wa kutumia alama ya kidole.

Tecno Camon i Sky ina dhamana ya siku 100 iwapo utataka ubadilishiwe simu, ruhusa ya kubadilishiwa kioo mara moja tu bila gharama yoyote na mwezi mmoja wa nyongeza kwenye dhamana.

Simu janja nyingine

Bei yake ni $113|Tsh. 254,250 (kwa bei ya ughaibuni).

Leo tumeiangazia Tecno Camon i Sky, unauzungumziaje uchambuzi wa kina kuhusi simu hii? Je, kuna simu ambayo ungependa kujua sifa/uwezo wake? Tuandikie kwenye sehemu ya kutoa maoni hapo chini.

Vyanzo: Gadgets 360, The Indian Express

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|