Tegemea Kuweza Kutumia Apps za Android kwenye Kompyuta

0
Sambaza

Katika moja ya maamuzi mazuri sana yaliyokuwa yanategemewa kwa muda mrefu sana Google wamerahisisha apps za Android kuweza kufanya kazi kwenye kompyuta. Kama unakivinjari cha Chrome basi tegemea kuweza kutumia apps mbalimbali hivi karibuni zinazopatikana kwa ajili ya Android.

Tayari Google walishawezesha baadhi ya apps kama vile Evernote kuweza kutumika katika programu endeshaji yao ya Chrome OS lakini kwa sasa wanawezesha apps zozote kuweza kupatikana katika soko la apps la kivinjari (browser) yao ya Chrome katika kompyuta za Windows, Mac na Linux.

SOMA PIA:  WhatsApp yatoa seti ya emoji zake mpya katika Toleo la WhatsApp Beta v2.17.364

Kupitia teknolojia waliotambulisha kama ARC – App Runtime for Chrome, watengenezaji wa apps za Android watawezeshwa kufanya mabadiliko machache tuu kupitia programu ya ARC kuwezesha apps hizo kuweza kufanya kazi katika kompyuta yeyote yenye kivinjari cha Chrome. Mabadiliko hayo ni kama vile kuwezesha utumiaji wa Kipanya na kibodi.

Muonekano wa app ya Flipboard ya Android Ikifanya kazi Kwenye Kompyuta

Muonekano wa app ya Flipboard ya Android Ikifanya kazi Kwenye Kompyuta

Tayari kuna apps (extensions) mbalimbali ambazo unaweza kuzipata kwenye soko la apps la Chrome basi tegemea kuweza kuzipata app mbalimbali za Android pia.

SOMA PIA:  Backup and Sync: App/Programu Mpya ya Google Drive yaja

Google wamepewa sifa kubwa sana kwa uamuzi kwani unazidi kukifanya kivinjari cha Chrome kuwa maarufu na chenye sifa za kipekee zaidi. Habari njema ni kwamba muda si mrefu utaweza kutumia apps zaidi ya milioni moja hii ikiwa ni pamoja na magemu na zingine nyingi zinazotengenezwa kwa ajili ya Android.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com