Tetesi: iPhone na iPads za Zamani Kupata Toleo Jipya la iOS 9

0
Sambaza

Hii itakuwa ni habari njema sana kwa watumiaji wengi wa simu za iPhones za matoleo ya nyuma kidogo kama vile iPhone 4. Inasemekena matoleo ya nyuma zaidi ndiyo yanauzika zaidi katika nchi zinazoendelea kama vile Tanzania, habari njema ni kwamba watumiaji wa matoleo haya wasiwe na wasi wasi wa kukosa toleo lijalo la programu endeshaji ya Apple, ifahamikayo kama iOS 9.

Mara nyingi matoleo mapya ya iOS yamekuwa yakiziacha simu za zamani solemba, na pale unapoweza kuweka toleo jipya basi unaweza kukuta linaathiri utendaji wa simu husika kwa kiasi kikubwa. Hili limetokea pia kwa simu za iPhone 4 baada ya mtu kufanya uamuzi wa kusasisha (update) simu hiyo kwenda toleo la iOS 8.

Toleo la iOS 9 linategemea kutambulishwa mwanzoni mwa mwezi wa sita
Toleo la iOS 9 linategemea kutambulishwa mwanzoni mwa mwezi wa sita

iOS ni programu endeshaji inayotengenezwa na kampuni ya Apple na inatumika katika vifaa vyake kama vile simu za iPhone, tableti za iPad na saa za iWatch.

Inasemekana katika toleo la iOS 9 litakalotambulishwa rasmi siku si nyingi kampuni ya Apple imefanya mabadiliko makubwa sana katika iOS kwa kuifanya kuwa nyepesi zaidi na kufanya kazi kwa urahisi zaidi ata kwenye simu au tableti za iPad zilizotoka kipindi cha nyuma kidogo. Bado haijajulikana ni matoleo gani ya nyuma ya iPhone na iPad yataweza kupata msasisho wa iOS 9 ila inasemekana ni matoleo mengi yaliyokuwa hayatarajiwi kufikiriwa yatakuwemo.

SOMA PIA:  iCloud kuhamia China, Je itakuwa kwa kila mtumiaji? Fahamu zaidi

Toleo la iOS 9 linategemea kutambulishwa mwanzoni mwa mwezi wa sita, endelea kutembelea TeknoKona na utafahamu yapi mapya yanakuja katika programu endeshaji hiyo.

Endelea kutembelea mtandao wako namba moja wa habari za kiteknolojia na maujanja katika lugha ya Kiswahili. Kusoma habari mbalimbali kuhusu kampuni ya Apple BOFYA – Apple | TeknoKona

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com