Jicho Letu Katika TECNO Phantom 8 Na Samsung Galaxy Note 8!

0
Sambaza

Simu Janja siku hizi zinakuja huku zikiwa na maboresho ya hali ya juu; huyu akiweka kamera nzuri kampuni pinzani na yenyewe inafanya hivyo huku ikiongezea maboresho mengine.

Ni wazi kwamba simu za Samsung ndio zinazoongoza katika soko la dunia la simu. TECNO nao hawapo nyuma katika kuhakikisha wanampatia mteja kile kilicho bora zaidi.

Meonekano Wa Mbele Kati Ya Phantom 8 Na Galaxy Note 8

Meonekano Wa Mbele Kati Ya Phantom 8 Na Galaxy Note 8

Leo nataka kulinganisha simu hizi mbili kwa haraka haraka (TECNO Phantom 8 na Samsung Galaxy Note 8) ili ujionee yale yaliyomo ndani katika simu hizi.

Meonekano Wa Nyuma Kati Ya Phantom 8 Na Galaxy Note 8

Kilinganisho

Phantom 8

 Galaxy Note 8

RAM GB 6 GB 6
Mega Pixels (MP) Kamera Ya Mbele 20MP, Yenye Flash Mbili na Kamera Ya Nyuma Ziko Mbili 12MP + 13MP, Uwezo Wa Kuzoom Mara 10 Zaidi Kamera Ya Mbele 8MP na Kamera Ya Nyuma Ziko Mbili Zote Zikiwa Na 12MP lakini Kazi Ni Tofauti Tofauti.
Kamera Mbili? Ndio – Nyuma Ziko Mbili Ndio – Nyuma Ziko Mbili
Uwezo Wa Betri 3,500mAh – Haliwezi Toka 3,300mAh – Haliwezi Toka
Prosesa Octa core 2.6 GHz Octa-core (2.3GHz Quad +1.7GHz Quad), 64-bit, 10nm processor
Network  Inaruhusu Mpaka 4G Inaruhusu Mpaka 4G
Ujazo Wa Ndani (ROM) GB 64 GB 64
Memori Kadi? Inaruhusu Kuongeza Mpaka TB 2 Inaruhusu Kuongeza Mpaka GB 256
Uwezo Wa Kioo 1920*1080 FHD 1440 x 2960 pixels
Aina Ya Kioo IPS (LCD) AMOLED
Ukubwa Wa Kioo Inchi 5.7 Inchi 6.3
Utambuzi Wa Alama Za Vidole? Ndio – Upo Kwa Nyuma Ndio – Upo Kwa Nyuma
Rangi Zilizopo Champagne Gold, Phantom Black Na  Galaxy Blue
Midnight Black, Deepsea Blue, Orchid Gray Na Maple Gold
Ukubwa (Wembamba) 159.95 x 79.5 x 7,9 mm (wembamba 5.6mm) 162.5 x 74.8 x 8.6 mm (6.40 x 2.94 x 0.34 in)
Jumba Lake  Kioo Kikubwa Ambacho Kimezungukwa Na Umbo bapa la chuma Nyuma Na Mbele Kuna Kioo (Gorilla Glass 5) Pia Imezungukwa Na Fremu Ya Aluminiam.
Muonekano Wakati Wa kupiga Picha . Tecno Ikiwa Katika 'ReFocus' Wakati Note 8 Ikiwa Katika 'Live Focus'

Muonekano Wakati Wa kupiga Picha . Phantom 8 Ikiwa Katika ‘ReFocus’ Wakati Note 8 Ikiwa Katika ‘Live Focus’

Ukizitazama sifa za simu hizi mbili kwa umakini kabisa na kulingana na thamani ya pesa yako nina imani utajua kabisa ni ipi ya kuinunua.

Tofauti Ya Wembamba Kati Ya Simu Hizi Mbili

Simu zote mbili hizi ni kali  na ni za kisasa zaidi. Niandikie hapo chini sehemu ya comment. Wewe hili umelipokeaje? ningependa kusikia kutoka kwako.

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Jinsi ya kusambaza kitu chenye ujazo mkubwa kwenye WhatsApp #Maujanja
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com