FUNUNU:Twitter Mbioni Kutumia Maneno Zaidi Ya 140 Ktk Siku Za Usoni! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

FUNUNU:Twitter Mbioni Kutumia Maneno Zaidi Ya 140 Ktk Siku Za Usoni!

0
Sambaza

Twitter mbioni kuanza kutumia maeno zaidi ya 140. Hii limekua tatizo kwa watumiaji wengi wa mtandao wa twitter kwa mda mrefu. Kampuni la twitter limepata malalamiko na maoni mengi kutoka kwa watumiaji wa wadau mbalimbali wa mtandao huo wa kijamii.

purchase celexa online

a doctor's order is 0.125 mg of ampicillin. the liquid Pengine ndio maombi hayo ya watumiaji wa twitter yanafanyiwa kazi. Kwa taarifa za haraka haraka inasemekana kuwa Tweets zitaongezwa na kuwa herufi 10,000 ambazo zitaku sawa kabisa na namba ya herufi zitakazotumika katika sehemu ya ‘direct Message’ -DM (meseji). Ongezeko hili la idadi ya maneno katika Tweets linasemekana kuanza kutumika mwanzoni mwa mwaka huu na hii ni kutoka katika vianzo mbalimbali vya habari za teknolojia

TwitterJapokuwa muongeaji rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter Bw.Jim Prosser aligoma kuongea jambo lolote kuhusiana na fununu hizi.

go JINSI ITAKAVYOFANYA KAZI

  • Kama kawaida katika mtandao huo sehemu yake ya kuona Tweet za watu (timeline) utaweza kuona maneno 140 katika tweet kama kawaida lakini utaweza kuona maneno zaidi uki’click’ hiyo tweet

Mpango huu unafanyika ikiwa ni mpango madhubuti wa bwana  Jack Dorsey ambaye ni mtendaji mkuu wa mtandao wa twitter, katika kuhakikisha twitter inapata watumiaji wengi na kuwa mtawala katika mitandao ya kijamii

Swala la maandishi yenye idadi ya manen0 140 limewatesa wengi kwani imekuwa ikiwalazimu waandike zaidi ya tweet moja ili kueleweka. Tena kwa wale wasioweza kujielezea ni shida tupu!

“Nimeipa changamoto timu yangu nzima iangalie kwa jicho la tatu  katika kuangalia namna gani tunavyoweza kuufanya mtandao wa twitter kuwa bora zaidi katika ku’share’ na watu mambo mbali mbali yanayotokea – Alisema Bw. Jack Dorsey katika mkutano wa kampuni”

Inavyosemekana twitter imekua na ukuaji mdogo katika ongezeko la watumiaji wa mtandao huo. hivyo imewalazimu wafikirie ni namna gani ambayo wanaweza washawishi watu wengi wajiunge na mtandao huo wa twitter. Moja katika njia hizo inasemekana na kuongeza idadi ya maneno katika tweet itakua moja wapo

Hii ni jambo jema kutoka twitter likikamilika kwani watakua wamejibu vilio vingi vya watumiaji wake. Tuambie mawazo yako juu ya hili sehemu ya comment hapo chini. Tafadhali usisahau kuutembelea mtandao wako pendwa wa teknokona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply