Uganda Watengeneza Basi la Kutumia Umeme wa Jua

0
Sambaza

Sio mamtoni kama tulivyozoea, hii ni kutoka kwa majirani zetu. Huko Uganda wamefanikiwa kutengeneza na kutambulisha rasmi basi la viti 35 linalotembea kwa kutumia nguvu ya umeme jua (Solar energy).

Uganda wanazidi kuonesha ni kwa jinsi gani hawaishii kwenye kujifunza tuu kuhusu teknolojia bali wanaenda hatua za mbele zaidi – utengenezaji.

Uganda watengeneza basi

Basi hilo limetengenezwa na shirika la Kiira Motors Corporation (KMC), ambalo linapata luzuku kutoka serikali ya Uganda. Hili si gari la kwanza kutengenezwa na shirika hilo, na nia yao kubwa ni kuhakikisha wanapata wateja ili kuwawezesha kutengeneza na kuuza mabasi hayo.

SOMA PIA:  Uwekezaji wa Nokia kwenye afya na teknolojia ya VR

Kupitia mabetri mawili ya umeme wa ziada basi hili litaweza kutembea umbali wa kilomita 80 kwa kutumia chaji iliyopo na ata zaidi kutokana na mabetri hayo kuendelea kuchajiwa kupitia ‘solar panels’ zilizowekwa juu ya basi hilo.

airtel tanzania bando

basi-uganda-tengeneza-gari

Solar Panels zikiwa juu ya basi hilo

Wanategemea kufikia mwaka 2018 wataweza kuwa tayari kutengeneza na kuuza mabasi hayo kulingana na oda watakazozipata. Lakini ili kufikia hatua hiyo shirika hilo linaitaji pesa kutoka kwa wawekezaji wengine nje ya luzuku ya serikali ambayo ni kwa ajili ya utafiti zaidi.

SOMA PIA:  Space X yapata wateja wawili wa kwanza wa kwenda kwenye mwezi

$58,000 kwa basi moja!!!!!!!

Hiyo ndio bei wanayotegemea kuuzia mabasi hayo, hii ni bei ya juu bado ukilinganisha na kati ya $35,000 hadi $50,000 inayoweza kukupatia mabasi mapya kwa sasa yenye kiwango cha viti 35 vya kukaa. Dola 50,000 za kimarekani ni takribani Tsh Milioni 126 | Kes Milioni 5.9

Mmoja wa wahandisi wa shirika hilo, Doreen Orishaba amesema wanaendelea na utengenezaji huku wakisoma hali ya soko ili kuhakikisha ya kwamba hawaishii kutengeneza na kuonesha tuu bali wafanikiwe kiasi cha kuuza mabasi hayo. Na hili linaweza tokea kama hawataweza kutengeneza kwa kiwango bora na huku bei ikiwa chini ukilinganisha na ushindani uliopo sokoni.

SOMA PIA:  Miaka 10 ya MacBook Air: Urithi wa Jobs kwa ulimwengu wa teknolojia

Je una maoni gani juu wa maendelea wanayofikia katika utengenezaji wa magari? Tuambie kwenye eneo comment

Chanzo: BBC

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com