Ujumbe wa kejeli umekuwa msukumo mkubwa mtu kufanyiwa upasuaji

0
Sambaza

Masihara yaweza kuwa dhihaka lakini pia utani una faida zake mbali na kukufurahisha na kuongeza siku za kuishi duniani kiasi cha kumuwezesha askari mmoja nchini India kupatiwa matibabu.

Taarifa ya Twitter iliyotumwa na mwandishi maarufu wa India kumuaibisha polisi mmoja wa nchi hiyo kwa kuwa mnene kupindukia imekuwa na matokeo ambayo hayakutarajiwa; kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito mjini Mumbai bila malipo yoyote.

Inspekta Daulatram Jogawat akiwa hospitalini.

Mwandishi alituma ujumbe wa Twitter wa picha ya Bwana Jogawat mwezi uliopita, akisema kuwa polisi huyo aliyeko Mumbai alikuwa na mpango wa “kuweka usalama mzito” kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Ujumbe huo uliosambazwa sana na kupelekea hospitali ya Saifee kujitolea kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wake.

Insp. Daulatram Jogawat alipata fursa ya kwenda Mumbay kwa mara ya kwanza ajili ya matibabu kwa sababu ya ujumbe wa Twitter na kuongeza kuwa uzito wa mwili ulianza kuongezeka kutokana na matatizo ya kiafya, na si kwa sababu anakula sana.

Shobhaa De baadae alitetea ujumbe wake wa Twitter na kusema kuwa azma yake haikuwa kumuudhi yeyote.

Inspekta Jogawat anaendelea vema baada ya upasuaji, na uzito wa mwili wake unaweza kupungua hadi karibu kilo 80 katika mwaka ujao. Alikuwa na uzito wa kilo 180 kabla ya upasuaji.

Vyanzo: BBC, The Financial Express

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  HP yatoa kompyuta/tabiti ya kwanza ulimwenguni ambayo ni Workstation
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com