Utakachokiona Katika ‘News Feed’ Facebook Kitategemea Na Intaneti Yako!

1
Sambaza

Facebook wameboresha mambo mengi hivi karibuni. Wameongeza vipengele kibao kama vile facebook spesheli kwa watu wa maofisini n.k. Mambo yamekuwa ni mengi hasa kwa wale wanotumia facebook katika kompyuta. Sasa video za facebook zinajicheza zenyewe hata kama hujabofya alama ya ‘play’ sasa swali linakuja vipi kama una bando hafifu au intaneti yako sio ya kasi?

Sawa kuna Teknolojia mpya za 4G katika nchi mabali mbali lakini kumbuka watumiaji wengi wa simu ni wale wanaotumia 2G na 3G. Pia ‘News Feed’ ya facebook ni mahali ambapo pana mafaili mengi kama vile video,picha, status za kawaida n.k hivi vyote vinahitaji intaneti imara na yenye kasi kwa namna moja au nyingine. licha ya hivyo mtumiaji wa mtandao huu unaweza ukatumia mda mwingi ukiwa unasonya kuliko ukiwa unafanya mambo mengine katika mtandao huo.

SOMA PIA:  Namna ya kuzima Video zinazocheza zenyewe Facebook katika simu na Kompyuta

facebook-news-feed

Facebook wameboresha! mtumiaji wa mtandao huo atapata taarifa mbalimbali katika News Feed kulingana na intaneti yake, hii inamaanisha kama intaneti yako iko chini unaweza shangaa unoana picha na status za kawaida na mambo mengine ambayo hayahitaji intaneti yenye kasi sana kama vile video.

airtel tanzania bando

Kwa upande wa Facebook wamesema kuwa wanafanya yote haya ili kuhakikisha kila mtu anaweza kuingia katika mtandao huo kwa uwezo (spidi) ya intaneti yake.

Facebook wanafanya hivi pia ili kuongeza watumiaji wake. Huduma hii inatumiwa sana katika baadhi ya sehemu ambazo hakuna inteneti yenye spidi ya 4G, hivyo ni msaada mkubwa sana

SOMA PIA:  Twitter yaleta kipengele kipya kwenye mtandao wake

Tuambie unaonaje hili sehemu ya comment. Kwa habari za teknolojia kama hizi usisite kutembelea TeknoKonaDotCom kila siku. TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

1 Comment

  1. Pingback: Utakachokiona Katika ‘News Feed’ Facebook Kitategemea Na Intaneti Yako! | Teknolojia

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com