fbpx

Watumiaji wa WhatsApp kwenye iOS waletewa vitu vipya

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mara nyingi masasisho yanapotolewa basi simu zinazotumia Android ndio zinazokuwa za kwanza kupata masasisho na kufuatiwa na iOS baada ya muda kidogo lakini kwa sasisho hili limetolewa kwa wale iPhone.

WhatsApp, Facebook na Instagram zote zinamilikiwa na na kampuni moja, Facebook Inc. na sasa sasisho la WhatsApp toleo la 2.18.51 kwenye iPhone linawezesha watumiaji wa vifaa vya Apple kuweza kuangalia video za kwenye Instagram na Facebook hapohapo kwenye WhatsApp.

Kitu hicho kipya kwa wanaotumia WhatsApp kwenye iPhone wataweza kuangalia picha jongefu za kwenye Facebook/Instagram kupitia WhatsApp; mtumiaji hatakuwa anapelekwa kwenye programu tumishi husika kuweza kuangalia video husika.

Kwa takwimu zilizotolewa na Mark Zuckerberg alipokuwa akiongea kwenye onyesho la F8 alisema kuwa WhatsApp ina Watumiaji 450 milioni duniani kote na WhatsApp Business mpaka sasa ina watumiaji zaidi ya milioni 3 ulimwenguni kote.

Watumiaji wa WhatsApp

Kwa sasisho jipya kwenye iPhone mtu hataenda sehemu ambapo video video imechapishwa (kwenye Facebook/Instagram).

Vilevile, sasisho hilo linamuwezesha mtumiaji kuweza kuangalia video husika wakati huohuo ukiwa unaweza kuwa unatuma ujumbe kwa watu mwingine; unaweza ukaipandisha na kuishusha au hata kuisimamisha kwa muda.  Kitu hiki kinafana na kile ambacho unaweza kufanya wakati unaangalia video Youtube.

Kuwasiliana kwa wengi kwa wakati mmoja (mpaka watu wanne) kwa njia ya video ni kitu kipya ambacho kipo mbioni kuja kwenye WhatsApp. Masasisho haya yanakufanya uzidi kupenda kutumia WhatsApp?

Vyanzo: Gadgets 360, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Jumia na skendo ya kudanganya data kwa wawekezaji! Yakanusha!
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|