WhatsApp na Gmail, na apps 6 zingine zenye Watumiaji Bilioni moja na zaidi kwa Mwezi

0

Apps za WhatsApp na GMail zimeingia kwenye orodha ya app chache zinazotumiwa na zaidi ya watumiaji bilioni moja kila mwezi.

Katika orodha hiyo ya apps zenye zaidi ya watumiaji bilioni moja kwa mwezi apps za Google kwa sasa ni sita wakati Facebook imeingia app yake ya Facebook na app ya WhatsApp ambayo inamilikiwa na kampuni hiyo pia.

watumiaji bilioni moja apps-whatsapp-google-facebook-gmail

App ya Facebook ina wastani ya watumiaji bilioni 1.59 kila mwezi, wakati huduma zingine pia zenye wastani wa zaidi ya watumiaji bilioni 1 kwa mwezi ni huduma chini ya Google, – Google search, Chrome (kivinjari -simu na kompyuta), Google Maps, YouTube, na programu ya soko la apps Google Play (inayotumika kwenye Android).

Kwa kiasi kikubwa ununuaji wa app ya WhatsApp uliofanywa na Facebook miaka michache iliyopita ulisababishwa kwa kiasi kikubwa na kampuni ya Facebook kutambua ukuaji wa haraka wa watumiaji wa huduma ya WhatsApp. Ingawa huduma ya WhatsApp haitengenezi faida yeyote kwa sasa, Facebook wanaangalia mbali zaidi.

Endelea kutembelea mtandao wa TeknoKona kwa habari na maujanja mbalimbali yahusuyo Teknolojia mbalimbali

Picha na mtandao wa TheGuardian

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com