WhatsApp Yafikisha Watumiaji Milioni 800 Kwa Mwezi

WhatsApp Yafikisha Watumiaji Milioni 800 Kwa Mwezi

0
Sambaza

Bosi mkuu wa WhatsApp ameelezea mwishoni mwa wiki iliyopita ya kwamba WhatsApp imefanikia kupata mafanikio ya kuwa na wastani wa watumiaji milioni mia nane kila mwezi duniani kote.

Mkurugenzi huyo, Bwana Jan Koum, katika kusema hayo alikumbusha ya kwamba hawa ni watu wanaotumia app hiyo ndani ya mwenzi na si wale waliojiandikisha tuu. Hii inamaana ya kwamba waliojiandikisha watakuwa ni watu wengi zaidi lakini data muhimu zaidi ni kutambua idadi ya watu wanaotumia huduma hiyo mara kwa mara.

Wakati mkurugenzi huyu akisema haya Umoja wa Ulaya unampango wa kupitia na kufanya mabadiliko kwa sheria zinazosimamia na kuendesha biashara na teknolojia za kimawasiliano baada ya malalamiko ya muda mrefu kutoka makampuni makubwa ya simu ya nchi za umoja huo wanaoona WhatsApp, Skype na huduma zingine kama hizo kama washindani wao katika biashara.  Katika mabadiliko hayo wadau wengi wanategemea huduma kama WhatsApp, Skype kujikuta wakitakiwa pia kutoa huduma za bure kwa mawasiliano muhimu kama vile Polisi, Zima Moto n.k

INAYOHUSIANA  Facebook ina mbinu ya kuwa karibu na mkufunzi

WhatsApp iliyonunuliwa na kampuni ya Facebook kwa zaidi ya dola bilioni 19 mwezi wa kumi mwaka jana imejikuta ikizidi kufanya vizuri sana kiukuaji. Mwezi wa nane mwaka jana ilikuwa na wastani wa watumiaji milioni 600. Mwezi wa kwanza mwaka huu ilikuwa na wastani wa watumiaji milioni 700

Je vipi kuhusu mitandao kama Twitter, Instagram na Facebook.

  • Mwezi wa pili mtandao wa Twitter ulikuwa na wastani wa watumiaji milioni 288 kwa mwezi Disemba mwaka jana
  • Instagram ilitoa ripoti ya kwamba ina wastani wa watumiaji milioni 300 kwa mwezi
  • Facebook ambao ndio pia wamiliki wa Instagram na Twitter, kwenye data zao za Disemba 2014 mtandao wao wa Facebook ulikuwa na wastani wa watumiaji bilioni 1.39 kwa mwezi
INAYOHUSIANA  Intagram yaenda mbali, sasa inawatumiaji hai bilioni moja

Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya Teknolojia! Kumbuka kusambaza habari na maujanja kwa ndugu na marafiki!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply