Uwepo wa simu janja kwa miaka 25 #Ripoti

0
Sambaza

Simu janja ambazo ni maarufu sana katika karne hii ya 21 kutokana na kuweza kusaidia, kurahisisha kazi mbalimbali ambazo hivi sasa zinafanyika kidijiti zaidi na kuonyesha ukuaji wa kasi wa teknolojia.

Mpaka hivi leo tunazungumzia miaka ishirini na tano (25) tangu simu janja ya kwnza ilipotambulishwa mnamo mwaka 1992. Tangu mwaka 1992 na mpaka hivi leo kuna simu janja ambapo idadi kamili ni ngumu sana kufahamika kutokana na makampuni mengi tu kujishughulisha na biashara ya simu janja.

IBM Simon (Simon) ndio simu janja ya kwanza kutoka na kuwekwa katika kundi la kuwa simu janja ya kwanza duniani iliyotoka mwaka 1992. Sababu ya kuwa simu janja ni kuwa na programu tumishi kama ramani, pamoja na vitu vingine kwa simu janja (kwa wakati huo).

IBM Simon Vs Samsung Galaxy S8.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Global Data ambao walifanya utafiti wao kwa kulinganisha simu janja ya kwanza kabisa na simu janja iliyotoka mapema mwaka 2017 kutoka Samsung nikimaanisha Samsung Galaxy S8.Utafiti huo uliangazia uzito, wembamba, rangi, ubora wa kamera wa simu janja na bei zake kwa ujumla. Matokeo ya utafiti huo yalikuwa kama ifuatavyo:-

Rangi. Simu janja za siku hizi ni nyepesi mara tatu zaidi ya simu janja ya kwanza huku wembamba ukiwa ni karibu mara tano zaidi ya Simon (simu janja ya kwanza).

Ubora wa kamera. Kwa asilimia 400 imeonekana simu janja (Samsung Galaxy S8) imeonekana kuwa bora kwenye upande wa ubora wa picha, yaani vile vipande vidogo vidogo (pixels) ambavyo kwa pamoja vinaunda picha kamili.

Rangi. Upande wa rangi utakubaliana na nasi pamoja na Global Data kwamba simu janja za siku hizi zinakuja katika rangi tofauti tofauti tofauti na simu janja ya mwaka 1992 ambayo ilikuwa ikipatikana katika rangi moja tu ambayo ni nyeusi.

Simu janja Simon: Kwa muonekano tu ni kwamba ilikuwa ni nzito na hata kwa kiasi fulani kuwa changamoto kuihifadhi mfukoni.

Uhifadhi. Katika kipengele cha diski uhifadhi hapa maendeleo ni makubwa sana ambapo simu janja diski uhifadhi unaanzia kwenye GB (Gigabytes) na kuendelea tofauti na simu janja Simon ambayo ujazo wake wa juu kabisa ulikuwa ni MB 32.

Kasi ya kupakua vitu. Kwa simu janja kama Samsung Galaxy S8 kasi yake ya upakuaji vitu kutoka mtandaoni ni mara laki tano bora zaidi kuliko simu janja Simon ambayo kasi yake ya kupakua ni sawa na kasi ya kupakua kwenye modem.

Bei za simu janja. Hapa tofauti kati ya simu janja ya kwanza na bei ya Samsung Galaxy S8 si kubwa sana ambapo ongezeko lake ni sawa na 50%; hii inamaanisha simu janja Simon haikuwa bei rahisi na ukingatia ndio simu janja ya kwanza kabisa.

Takwimu za simu janja za sasa hvi na ile simu janja ya kwanza kabisa katika vipengele mbalimbali.

Kwa uwepo wa simu janja umebadilisha mambo mengi ambayo daima tutayakumbuka kutokana na mabadiliko hayo kuja maboresho/kitu kipya kila inapotoka simu janja mpya na kupata soko kutokana na kilichowavutia wateja ila tusisahau vya kale.

Chanzo: Global Data

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Ujumbe wa kejeli umekuwa msukumo mkubwa mtu kufanyiwa upasuaji
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com