´╗┐ Xiaomi wazindua simu mbili zenye kamera ya selfie yenye megapixel 16

Xiaomi wazindua simu mbili zenye kamera ya selfie yenye megapixel 16

0
Sambaza

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, leo kampuni ya Xiaomi imezindua Simu Janja mpya mbili za familia ya Y ambazo zitakuwa na kamera ya mbele (selfie) zenye megapixel 16. Simu janja hizo mbili zilizozinduliwa huko India ni Redmi Y1 na Xiaomi Redmi Y1 Lite.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo kameara hizo za mbele zina ubora mzuri na zitakuwa na uwezo wa kuingiza mwanga mkubwa pale picha inapotaka kuchukuliwa. Zitakuwa na flashi kwa ajili ya kusaidia penye mwanga hafifu.

Xiaomi Redmi Y1 na Xiaomi Redmi Y1 Lite zinatumia Android Nougat yenye MIUI 9 Beta ambapo itapata masasisho kuanzia katikati ya Novemba mwaka huu.

Sifa ya Xiaomi Redmi Y1

click here Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.1.2 Nougat yenye MIUI 9 Beta
http://seagullaerial.com/awards/ Kioo: Ukubwa wa inchi 5.5
cheap avodart uk Prosesa: 1.4 GHz Qualcomm Snapdragon 435 octa-core 64-bit
RAM: 3/4GB
Uhifadhi wa ndani: 32/64GB
Kamera ya mbele: MP 16
Kamera ya nyuma: MP 13
Betri: 3,080mAh

Simu janja mbili kutoka Xiaomi: Muonekano wa nyuma wa Redmi Y1.

Xiaomi Redmi Y1 itakuwa na aina mbili tofauti ya ujazo wa hifadhi wa ndani na ukubwa wa RAM. Moja itakuwa na 3GB + 32GB ambayo itauzwa kwa Dola 140|Tsh. 314,860 na nyingine ni 4GB + 64GB itauzwa kwa Dola za kimarekani 170|Tsh. 382,330.

INAYOHUSIANA  Bios Cube: Majivu ya marehemu kutumika kukuza mmea

Sifa ya Xiaomi Redmi Y1 Lite

Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.1.2 Nougat yenye MIUI 9 Beta
Kioo: Ukubwa wa inchi 5.5
Prosesa: 1.4 GHz Qualcomm Snapdragon 425 quad-core 64-bit
RAM: 2GB
Uhifadhi wa ndani: 16GB
Kamera ya mbele: MP 5
Kamera ya nyuma: MP 13
Betri: 3,080mAh

XIAOMI WAZINDUA SIMU MBILI

Simu janja mbili kutoka Xiaomi: Muonekano wa Redmi Y1 Lite

Simu ya Xiaomi Redmi Y1 Lite itauzwa kwa dola za kimarekani 115|Tsh. 258,635. Simu zote mbili unaweza kuweka memori kadi ya kubwa mpaka 128GB.

Simu zote hizo zitapatikana soko la Amazon kuanzia mchana wa Novemba 8, na baadae zitapatikana katika masoko mbalimbali duniani, ikiwemo maduka ya Xiaomi na washirika wake.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.