Kampeni ya kutaka watu wafute akaunti zao za Facebook yaanzishwa - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kampeni ya kutaka watu wafute akaunti zao za Facebook yaanzishwa

6
Sambaza

Baada ya Cambridge Analytica kugundulika kutumia taarifa za watu kwenye Facebook mengi yameibuka baada ya taarifa hiyo na sasa kampeni maalum ya kuwashawishi watu kuacha kutumia Facebook imeanza kama mwarobaini wa wao kuwa salama mtandaoni.

buy modafinil uk next day

source link Kampeni hiyo ya can i buy Phenytoin over the counter in spain #DeleteFacebook iliyoanzishwa na mwanzilishi mwenza wa WhatsApp, Bw. Brian Acton amekuwa mstari wa mbele kuhusu kampeni hiyo kwa kuwaambia watu ‘Waliomfuata’ kwenye ukurasa wake wa Twitter baada ya taarifa kuhusu Cambridge Analytica kutumia taarifa za watu kutoka Facebook.

Hatua hiyo ya kushawishi watu wafute akaunti zao za Facebook imekuaja baada ya Cambridge Analytica kutumia taarifa za watu (kwenye Facebook) takribani 50mil bila idhini yao.

Kitendo cha Cambridge Analytica kututumia taarifa za watu kutoka Facebook kimefanya mamlaka husika za Uingereza na Marekani kufikiria kuchunguza iwapo taarifa watu watu kutoka mataifa hayo mawili nazo zilichukuliwa bila idhini kutoka kwa wahusika.

 kutaka watu wafute akaunti zao za Facebook

Inadaiwa Cambridge walikusanya taarifa na kufanya upembuzi yakinifu ambapo zilipelekea rais Trump kumshinda mpenzani wake kwa tofauti ya kura 40 elfu katika majimbo matatu.

Afrika nayo imekubwa na mkono wa Cambridge Analytica, nchini Kenya tayari wabunge wameomba uchunguzi ufanyike kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 iwapo kampuni hiyo ilihusika kumsaidia rais Uhuru Kenyatta kushinda katika uchaguzi huo.

Je, unafikiri ukifuta akaunti yako ya Facebook ndio itakuwa suluhisho la taaarifa za watu kutumiwa bila idhini? Tupe maoni yako.

Vyanzo: Gadgets 360, The Times of India

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Biashara ya kwanza kufanyika mtandaoni
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|