´╗┐ Miaka 10 ya MacBook Air: Urithi wa Jobs kwa ulimwengu wa teknolojia - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Miaka 10 ya MacBook Air: Urithi wa Jobs kwa ulimwengu wa teknolojia

0
Sambaza

Kamwe dunia hawezi kusahau mchango wa moja kati ya watu walioleta mageuzi katika sekta ya teknolojia na kufanya vitu kama kompyuta kupendwa zaidi na kwa hakika zitaendelea kutumika. Steve Jobs alifanya mengi ambayo ni wachache sana wenye uwezo huo.

Kompyuta aina ya MacBook Air ambazo zipo chini ya Apple (kampuni) mwaka 2018 inatimiza miaka 10 tangu hapo marehemu Steve Jobs alipoitambulisha kompyuta ya kwanza toleo la MacBook Air mwaka 2008 na kuifanya kompyuta hiyo kuwa maarufu tangu hapo na mpaka hivi leo.

Kwanini MacBook Air ni urithi kwa dunia aliouacha Jobs?

Kompyuta za wakati huo zilizokuwepo tayari sokoni mwaka 2008 kurudi nyuma karibu zote zilikuwa na sifa zinazofana; click zilikuwa na wembamba wa karibu inchi moja, uzito wake ukiwa Kg 3.18, ukubwa wa vioo vya kompyuta hizo ulikuwa kati ya inchi 8-11 na nyingi kati ya kompyuta hizo hazikuwa na keyboard ambayo imejaa katika eneo lake.

Miaka 10 ya MacBook Air: Mwaka 2008 MacBook Air ilikuwa ikiuzwa kwa $1,799|Tsh. 4,047,750

Mageuzi yaliyokuja kufanywa na Jobs kwa kuleta MacBook Air kwa ulimwengu yalibadilisha kabisa taswira ya kompyuta kutokana na kompyuta hizo kuwa see nyembamba sana Apple iliachana kuweka sehemu ya CD Drive, kutumia diski uhifadhi za SSD, kutumia vidole viwili kutembeza kipanya, kuwa na sehemu moja tu ya USB 2.0, shehemu ya kuchomeka DVI na kuwa na sehemu ya kuchomekea spika za nje.

Katika uzinduzi wa wa MacBook Air mwaka 2008 marehemu Steve Jobs aliitambulisha kompyuta hiyo kutoka kwenye bahasha nyembaba sana jambo ambalo liliwashangaza watazamaji waliohudhuria kwenye uzinduzi huo wa MacBook Air.

Sony VAIO X505 (2004) ndio ilikuwa nyembaba zaidi kwa wakati huo mpaka pale MacBook ilipokuja mwaka 2008.

SIo miaka mingi sana iliyopita washindani wa Apple nao walipoanza kutengeza kompyuta ambazo zinafana kwa umbo na hata baadhi ya sifa za ndani za kompyuta hizo. http://epetsure.com/2016/03/pet-poisons-look-easter-weekend/ Apple ilikataa kuunda upya MacBook Air ili kuweza kuleta ushindani na kompyuta kama vile Dell XPS 13 na badala yake ikatoa MacBook ya inchi 12, 13.

INAYOHUSIANA  Google Calendar yaongezewa vipengele vizuri sana

Mpaka hivi leo MacBook Air ni moja ya kompyuta bora na ghali, hivi sasa MacBook Air ya bei ya chini kabisa inaanzia $999|Tsh. 2,247,750. Alichokifikiria Jobs miaka 10 iliyopita ndio tunu miaka ya karibuni kwa washindani wakubwa wa Apple. Pumzika kwa amani Steve Jobs.

Vyanzo: The verge, Apple Insider, MacRumors

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.