Tigo Tanzania na Tecno wajisogeza karibu kwa wateja wake - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Tigo Tanzania na Tecno wajisogeza karibu kwa wateja wake

0
Sambaza

Tecno ni moja kati bidhaa (simu janja) zilizoenea barani Afrika kwa wingi na kufanya kuwa na soko zuri barani humo lakini halikadhalika Tigo Tanzania nao wamekuwa wakijidhatiti ili kuweza kuendelea kufanya vizuri katika soko lenye ushindani na hatimae wasipoteze wateja.

Sote tunafahamu jinsi gani Tigo Tanzania ilivyokuwa na wateja wengi na kuzidi kuendelea kuwavutia watu wengine kila siku. Hivi karibuni Tigo Tanzania na Tecno wamua kushirikiana kwa faida ya wao na wateja wa bidhaa zao.

Siunafahamu simu janja mpya ya Tecno Camon X? Basi Tecno na Tigo Tanzania wanasema kwa kila mteja atakayenunua simu hiyo atakuwa anapata GB 3 za kifurushi cha intaneti BURE kila mwezi kwa muda wa miezi sita.

Tigo Tanzania na Tecno

Wawakilishi kutoka Tigo Tanzania na Tecno wakiongea na waandishi wa habari kueleza umma watakachokuwa wakifanya.

Ambacho pengine hukifahamu……

Tecno wameamua kufanya kazi na Tigo Tanzania kwa sababu ya Tigo kuwa na intaneti ya 4G katika maeneo mengi nchini humo (Tanzania) na isitoshe simu ya Tecno Camon X ina mfumo wa 4G hivyo kufanya wateja wake kufurahia intaneti yenye kasi kutoka Tigo Tanzania.

Tigo Tanzania na Tecno

Simu janja ya Tecno Camon X

Tigo Tanzania ndio kampuni ya ya kwanza ya mawasiliano kuweza kuleta simu hizo katika maduka yake yote yaliyopo katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Vilevile, see url mteja anaweza kununua simu janja ya Tecno Camon X kwa kulipa kidogo kidogo; unapiga *147*00# kisha utafuata maelekezo au kununua kupitia order avodart canada MTANDAONI.

Tecno Camon X inauzwa Tsh. 469,999 katika maduka yote ya Tigo ambapo simu hiyo itakuwa na kifurushi cha GB 3 za bure kila mwezi kwa siku 180. Bofya real Lamictal without prescription HAPA kujua sifa ya simu hiyo pamoja na mengineyo.

Chanzo: Tigo Tanzania

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Umoja wa Ulaya kudhibiti gharama za simu
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.