fbpx

Undani wa Nokia 8 na kupata masasisho ya Android 8.0

0

Sambaza

Ndani ya mwaka huu (2017) tu Nokia imetoa simu sizizopungua tano katika hali ya kuifanya simu za Nokia zinarudi katika umaarufu wake iliyokuwa nayo zamani na kuleta ushindani kwa makampuni mengine.

Nokia 8 ni moja kati ya ule muendelezo wa simu za Nokia kutoka Nokia 1, 2, 3….mpaka 9 na wakati Nokia 8 inatoka haikuwa na toleo la Oreo (Android 8.0), toleo ambalo mpaka sasa si simu janja zote za Android zimepata sasisho hilo. Kwa wenye Nokia 8 ni wakati wa kufurahi kwani simu hizo sasa zinaweza kufanya can i buy Premarin over the counter in spain masasisho na kuwa na Android 8.0.

Sasisho la Oreo kwenye Nokia 8. Simu janja za Nokia 1, 2, n.k zinatarajiwa kupata sasisho hilo hivi karibuni.

Je, Nokia 8 ina sifa gani?

HMD Global ambao ndio watengenezaji wa simu za Nokia hivi sasa na Nokia 8 ina sifa nyingi za kuvutia simu hiyo jambo ambalo ni jema kabisa baada ya see simu zake zilizokuwa zikitengenezwa na Microsoft kuifanya kampuni hiyo kuyumba kabisa kwenye biashara ya simu janja. Nokia 8 ilizinduliwa mwezi Agosti 2017 na kuanza kuuzwa duniani kote mwezi Oktoba 2017. Sifa za Nokia 8 ni kama ifuatavyo:-

INAYOHUSIANA  Vipya kutoka BlackBerry na Alcatel kuja karibuni

1. Prosesa/Kioo.

Simu janja Nokia 8 ina moja ya prosesa za kisasa kabisa na zenye nguvu iitwayo Qualcomm Snapdragon 835 SoC ambapo kasi yake ya kufanya kazi ni mpaka 2.5 GHz Kryo na 4×1.8 GHz Kryo. Upande wa kioo kina ukubwa wa inchi 5.3 QHD na ikitokea akaidondosha Nokia 8 si rahisi kuvunjika kwa sababu inatumia teknolojia ya kisasa katika vioo vya simu janja nikimaanisha buy cheap viagra online australia Corning Gorilla Glass 5.

2. Kamera/Diski uhifahi.

Nokia 8 ina kamera 2; kamera ya mbele (mahususi kwa selfie) na ile ya nyuma ila cha kuvutia kuhusu simu hii kwenye upande wa kamera ni kwamba zote zina ubora uleule picha kwa maana ya kwamba kamera ya mbele na nyuma zote zina MP 13.

Kwenye diski uhifadhi mtumiaji anaweza asiwe na haja ya kuweka ujazo wa ziada; Nokia 8 inakubali SD card ya mpaka GB 256 lakini ujazo wa kwenye simu janja Nokia 8 ni GB 64.

3. Utambuzi wa alama za vidole/Bei yake

Ulinzi madhubuti kwenye simu janja ni kipaombele katika makampuni mengi makubwa yanayojishughulisha na biashara ya simu janja na teknolojia ya utambuzi wa alama za vidole imeshika kasi kwa sasa na kwenye Nokia 8 teknolojia hii ipo sehemu ya mbele na si myuma kama simu nyingi za Android. Bei yake ni $715|Tsh. 1,608,750.

Nokia 8 ni simu yenye uwezo wa hali ya juu na ukizingatia ina teknolojia ya Fast charging pamoja na NFC.

Sifa nyinginezo

Sifa

Uwezo

 RAM GB 4 (ya 64 GB diski uhifadhi) na 6 GB (ya GB 128 diski uhifadhi)
 Uwezo Wa Betri Li-Ion 3090mAh ambalo haliwezi kutolewa ndani ya simu na linakaa na chaji kwa saa 78
Uwezo Wa Kioo  1440×2560 pixels
Laini za simu Inakubali laini 2
Wembamba  151.5×73.7×7.9mm
Sehemu ya kuchomeka spika za masikioni Ina ukubwa wa 3.5mm
Rangi Tempered Blue, Polished Blue, Steel, Polished Copper
Network/Teknolojia nyinginezo 4G VoLTE, Wi-Fi 802.11ac, Bluetooth v5.0, GPS/A-GPS, USB Type-C (v3.1), haina redio
INAYOHUSIANA  Kutuma jumbe za kawaida kupitia tovuti

Sasisho la Oreo lina ukubwa wa MB 1518 hivyo ni vyema ukahakikisha kuwa una kifurushi cha kutosha kabla ya kuanza kuingiza sasisho hilo kwenye simu janja ya Android.

Vyanzo: Gadgets 360, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.